Makubaliano hayo yanataka mataifa 20 ya Serikali na maofisi kufanya kazi pamoja kuhakikisha taarifa zenye uhakika kuhusu matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa yanapatikana ili kuimarisha usalama wa taifa .
Museveni alisema mada hiyo imejiri wakati mwafaka kwani sehemu ndogo tu ya dunia, hususan katika nchi za Magharibi, zinafurahia utajiri ilhali maeneo mengi duniani, ikiwemo nchi ya Uganda, yanaathirika na umaskini.
Rais Obama ameelezea kuvunjika kwa makubaliano ya msingi mashariki ya kati na kusema jamii zimegubikwa na kutokuwa na uthabiti na utulivu.
Watu milioni 65 idadi ambayo haijawahi kutokea wamelazimika kukatisha maeneo mbalimbali duniani kutokana na mgogoro, umaskini uliokithiri na wengi kutokana na majanga ya kiasili.
Naibu huyo wa rais alikuwa mmoja wa waliozungumza katika kikao kilichoitishwa kwa minajiri ya kutafuta suluhisho la kudumu kwa mzozo wa uhamaji wa halaiki ya wakimbizi kutoka maeneo yaliyokumbwa na vita na migogoro ya kisiasa, zikiweno nchi za Syria na Somalia.