Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 24, 2023 Local time: 16:58

Wakazi wa Khartoum watumia muda wa utulivu kuzika jamaa zao


Moshi ukifuka katika eneo loliloko kusini mwa Khartoum tarehe 12 Juni 2023.

Familia na jamaa za watu waliouawa katika mapigano nchini Sudan Jumapili walianza kuzika maiti za watu zilizokuwa ziko katika hospitali ya Khartoum, huku mapigano makali na milio ya risasi ikianza punde baada ya muda wa sitisho la mapigano la saa 24 kumalizika.

Mapigano yamekuwa yakiendelea katika nchi hiyo iliyoko kaskazini-mashariki mwa Afrika, tangu katikati ya mwezi Aprili, wakati mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani Mohamed Hamdan Dagalo, anayeongoza kikosi cha kijeshi cha Rapid Support Forces, walipoanza kushambuliana.

Mfululizo wa makubaliano ya hivi karibuni ya kusitisha mapigano yaliwawezesha raia waliokwama katika mji mkuu wa Khartoum kwenda nje kukusanya chakula na mahitaji mengine muhimu.

Lakini siku ya Jumapili walikusanyika katika uwanja wenye changarawe ulioko kusini mwa mji mkuu wa Sudan ili kuwazika watu waliouawa kutokana na mashambulio ya mizinga.

Shahidi mmoja aliliambia shirika la habari la AFP kuwa katika kipindi cha dakila 10 tu, punde baada ya kumalizika kwa makubaliano hayo, saa kumi na mbili asubuhi siku ya Jumapili, jiji hilo lilitikiswa tena na mashambulizi ya makombora.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG