Mazungumzo kuhusu mpango wa kusitisha mapigano katika mzozo wa Gaza yanaonekana kuwa katika hatua za mwisho, na Rais wa Marekani, Joe Biden na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, watajadili mianya iliyosalia leo hii Alhamisi, afisa mkuu wa Marekani amesema Jumatano.