Kikao hicho ambacho hufanyika kila mwaka wakati unaokaribia siku kuu muhimu ya Ireland ya St Patrick’s, kwa kawaida huzungumzia masuala ya moja kwa moja kati ya Marekani na Ireland. Trump wakati akiketi kando ya Martin kwenye ofisi yake ya Oval huko White House, alisema kwamba “Kwa hakika tutajibu ushuru uliotangazwa na Umoja wa Ulaya ambao Ireland ni mwanachama, na kwamba Aprili 2 itakuwa mwanzo wa ushuru wa majibu kutoka Marekani."
Alisema kwamba Ireland imechukua makampuni mengi ya kutengeneza dawa ya Marekani kwa ajiri ya ushuru mdogo, akiambia Martin kwamba ingawa anaheshimu uamuzi huo, anahisi viongozi wa Marekani wangechukua hatua kuzuia makampuni ya Marekani kuhamia kwenye mataifa ya nje. Alisema kuwa anatazamia kufanya kazi na Ireland ingawa tofauti kubwa ya kibiashara iliyopo ni lazima ishughulikiwe.
Martin alipongeza Trump kwa kuwekeza kwenye uwanja wa golf mjini Doonbed, Ireland, akisema kuwa ndiye Rais pekee aliyewahi kufanya hivyo. Martin pia alisema kwamba makampuni ya kutengeneza dawa kama ile kubwa ya Eli Lilly, yenye operesheni nyingi Ireland yanaheshimu wafanyakazi wenye ujuzi na uzalishaji wa juu nchini mwake, lakini pia imetangaza mpango wa kuwekeza zaidi hapa Marekani.
Kampuni hiyo yenye makao yake makuu Indianapolis Marekani imetangaza mpango wa kuwekeza kwenye viwanda vine vipya hapa Marekani ikiwa mara mbili ya uwekezaji uliotangazwa 2020 wa hadi dola bilioni 50.
Forum