Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 09, 2024 Local time: 04:21

Tume huru zinazofuatilia uchaguzi DRC zinakiri kuwepo makosa kwenye uchaguzi


Mfano wa masanduku ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika DRC.
Mfano wa masanduku ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika DRC.

Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiprotestanti wamesema wamepokea ripoti 5,402 za matukio katika vituo vya kupigia kura ambayo yaliingilia kati zoezi hilo.

Katika ripoti mpya ya uchaguzi wa rais na bunge kulingana na maelezo kutoka kwa maelfu ya wafuatiliaji, tume huru ya pamoja zinazofuatilia kura huko Congo zenye nguvu katika Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiprotestanti, wamesema kuwa wamepokea ripoti 5,402 za matukio katika vituo vya kupigia kura ambapo zaidi ya asilimia 60 ya matukio hayo yaliingilia kati upigaji kura. Ujumbe huo “uliorodhesha makosa kadhaa ambayo yanaweza kuathiri uadilifu wa matokeo” ilisema.

Wakati huo huo serikali ya Congo siku ya Alhamisi ilikataa wito wa upinzani wa kufanyika tena kwa uchaguzi uliokumbwa na utata, wakati ujumbe mkuu wa waangalizi ukiripoti kuwepo “makosa mengi” ambayo yanaweza kudhoofisha baadhi ya matokeo.

Mabango ya kampeni za Rais Felix Tshisekedi mjini Kinshasa. December 13, 2023. (Photo by JOHN WE
Mabango ya kampeni za Rais Felix Tshisekedi mjini Kinshasa. December 13, 2023. (Photo by JOHN WE

Matokeo ya awali yaliyotolewa hadi sasa kutoka uchaguzi mkuu wa Desemba 20 yanaonyesha Rais Felix Tshisekedi anaongoza, lakini wapinzani wake wametaka matokeo yabatilishwe wakieleza masuala mapana yaliyojitokeza yanayopelekea kuahirishwa kwa uchaguzi.

Mzozo huo unatishia kuiyumbisha zaidi Kongo, ambayo tayari inakabiliwa na mgogoro wa usalama katika maeneo ya mashariki. Congo ni mzalishaji mkubwa duniani wa madini ya cobalt na madini mengine ya viwandani pamoja na shaba.

Forum

XS
SM
MD
LG