Wajumbe wanne kati ya saba walio na mamlaka ya kupiga kura walisema Jumanne kwamba wamemchagua Fritz Bélizaire kama waziri mkuu. Wananchi wengi wa Haiti walishangazwa na tamko lao na muungano wa kisiasa ambao haukutarajiwa.
Wanachama wa baraza wanaompinga Bélizaire sasa wanatafakari nini cha kufanya, ikiwemo uwezekano wa kupinga uamuzi huo au kujiuzulu kutoka kwa baraza hilo.
Bélizaire aliwahi kuwa waziri wa michezo wa Haiti wakati wa uongozi wa rais wa pili wa nchi hiyo, René Préval, kuanzia 2006 hadi 2011.
Forum