Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 05, 2024 Local time: 14:11

Baraza jipya la mpito la Haiti laapishwa Alhamisi


Wanajeshi wakiwa nje ya ofisi ya waziri mkuu ambapo baraza la mpito limeapishwa Alhamisi. Aptili 25, 2024.
Wanajeshi wakiwa nje ya ofisi ya waziri mkuu ambapo baraza la mpito limeapishwa Alhamisi. Aptili 25, 2024.

Waziri mkuu wa Haiti anayeondoka madarakani Ariel Henry kupitia taarifa ya Jumatano amesema kuwa baraza la mpito litaapishwa Alhamisi kwenye afisi za Waziri mkuu iliyoko katika viunga vya mji mkuu wa Port-au-Prince.

Baraza hilo lenye wajumbe 9 litakuwa na jukumu la kuteua waziri mkuu mpya pamoja na kubuni serikali mpya, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu. Henry alitangaza kujiuzulu kwake hapo Machi kufuatia kuzuka kwa ghasia kutoka kwa magenge kwenye mji huo mkuu wa Haiti.

Kiongozi huyo anayeondoka tayari ameomba msaada wa kimataifa ili kukabiliana na makundi hayo ambayo yanadhibiti takriban asilimia 80 ya Port-au-Prince.

Forum

XS
SM
MD
LG