Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 14:35

Tanzania yapoteza nafasi ya kuandika historia ya kupata ushindi wake wa kwanza AFCON


Wachezaji wa timu ya taofa ya Tanzania -Taifa Stars.
Wachezaji wa timu ya taofa ya Tanzania -Taifa Stars.

Timu ya taifa ya Tanzania ilipoteza nafasi ya kuandika historia ya kupata ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Afcon dhidi ya Zambia waliokuwa wamebaki na wachezaji 10 katika mechi ya kundi D na kutoka sare ya bao 1-1 katika uwanja wa San Pedro Ivory Coast.

Bao pekee la Tanzania lilifungwa na Mshambuliaji Simon Msuva katika dakika ya 11 baada ya kupiga shuti kali baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mbwana Samatta na golikipa wa Zambia Mulenga akashindwa kulizuia.

Mshambuliaji wa Leicester Patson Daka alisawazisha bao hilo katika dakika ya 88 akiunganisha kona ya Clatous Chama na kufufua matumaini ya timu yake kutinga hatua ya 16 bora.

Zambia ilibidi wacheze kipindi cha pili chote na wachezaji 10 baada ya beki wao Rodrick Kabwe kumfanyia madhambi Mbwana Samatta katika dakika ya 44.

Zambia iliwaingiza Ckatous Chama na Kennedy Musonda ambao walileta uhai katka timu hiyo iliyokuwa na wachezaji 10 na hatimaye kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika za mwisho za mchezo huo mkali.

Na katika mchezo wa awali wa Kundi D timu ya DRC iliwanyima fursa vigogo wa Afrika Morocco kupata alama tatu za kujihakikishia Kwenda raundi ya pili baada ya kutoka sare kwa bao 1-1.

Achraf Hakimi alikuwa ameipa Atlas Lions uongozi katika dakika ya 6.

na kuipa matumaini ya ushimndi lakini furaha yao ilizimwa katika dakika za jioni kama walivyofanya Zambia dhidi ya Tanzania ambapo Bao la kusawazisha la Silas Mvumpa lilihakikisha kuwa Congo wanaibana Morocco na kutoka sare kwa sare ya bao 1-1.

Mpaka sasa Morocco anaongoza kundi D akiwa na pointi 4 akifuatiwa na DRC na Zambia wenye pointi 2 na Tanzania inashika mkia na pointi moja.

Forum

XS
SM
MD
LG