Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 05:14

Wenyeji wa BAL AS Douanes ya Senegal waanza vibaya michuano hiyo


Mechi ya ufunguzi wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika msimu wa tatu kati ya ABC Fighters ya Ivory Coast na AS Douanes ya Senegal Machi 11, 2023.
Mechi ya ufunguzi wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika msimu wa tatu kati ya ABC Fighters ya Ivory Coast na AS Douanes ya Senegal Machi 11, 2023.

Timu ya nyumbani katika kanda ya Sahara AS Douanes ya Senegal na washiriki wapya wa BAL Abidjan Basketball Club (ABC) ya Ivory Coast walipambana vikali  katika mchezo wa ufunguzi wa msimu huu wa 3 wa BAL katika uwanja wa Dakar Arena Senegal.

Mshambuliaji wa ABC Mike Fofana alifunga kikapu cha kwanza cha msimu wa 2023 wa BAL kabla ya mchezaji wa zamani wa Chuo Kikuu cha Memphis Chris Crawford kujibu kwa kikapu na kupachika pointi zake za kwanza za msimu kwa timu ya AS Douanes. Baada ya timu hizo kumenyana katika mechi ya kwanza siku ya Jumamosi . Timu ya ABC waliendelea na msururu wa vikapu wakichochewa na pointi 8 kutoka kwa Fofana na safu kali ya ulinzi iliyoongozwa na Christopher Obekpa, ambaye uzuiaji wake mara 3 katika robo ya kwanza ulisaidia kujenga uongozi wa pointi 25-14 kuelekea robo ya pili.

Jean Jacques Boissy wa AS Douanes alianza kota ya pili kwa kupachika pointi tatu kabla ya ABC kupachika 8-bila majibu na kupanda hadi pointi 32 kwa 17. Pointi 3 za Crawford na dunk iliyowekwa na mchezaji anayechipukia kwenye BAL Khaman Maluach ziliamsha umati wa watu kwenye uwanja wa nyumbani. ABC waliendelea kuongoza kwa pointi za tarakimu mbili kwa sehemu kubwa ya kota hiyo kwa sababu ya mchezaji Abdoulaye Harouna aliyepachika pointi 12 katika kipindi cha kwanza, na mchezaji wa kati Alex Robinson Jr. ambaye alitoa asisti 4 kati ya assisti 11 za kipindi cha kwanza za ABC na kwenda mapumziko wakiwa na pointi 43-31.

Harouna alianza kota ya 3 vyema pale alipoishia ambapo alipachika pointi 3 ili kuendeleza uongozi wa ABC hadi 15 katika dakika za mwanzo za kipindi hicho. Mchezaji mwenye umbo kubwa wa NBA Academy Afrika, Maluach alijibu kwa pointi 3 baada ya kuongoza kwa kuchukua rebaundi 5 kwa timu ya AS Douanes katika kipindi cha kwanza. Timu hizo ziliendelea kushambuliana na kufunga vikapu katika kipindi chote cha kota ya tatu huku kinara wa pointi wa BAL mara mbili Terrel Stoglin akiikabili AS Douanes kwa pointi 7 katika kota ya tatu na kuiweka juu timu yake. Pointi 11 za Harouna, ambazo zilijumuisha pointi tatu mfululizo, ziliiweka ABC mbele kwa jumla ya pointi 58-48 katika kota ya mwisho.

ABC ilidumisha uongozi wake kwa muda mrefu wa kota ya 4 hadi kupachika pointi 12 kwa 2 ambayo ilijumuisha kikapu cha Ifeanyi-chukwu Ocher-eobia, na pointi tatu tatu kila mmoja kutoka kwa Crawford na Stoglin zilizusha furaha kwa mashabiki wa AS Douanes na kuwaweka karibu ndani ya pointi mbili tu na wapinzani wao. Lakini pointi za mipira ya adhabu za Harouna na pointi tatu za Fofana ziliendeleza uongozi wa ABC kurudi tena katika pointi 7 huku zikiwa zimesalia dakika mbili kabla ya mchezo kumalizika na kushinda kwa jumla ya pointi 76-70. Harouna aliongoza kwa ufungaji akipachika jumla ya pointi 25 huku Fofana akipachika pointi 21. Obekpa alifanya karibu kila kitu kwa ABC, akiongoza timu katika reboundi 9, asisti 5 na kuzuia 3. Stoglin na Crawford walipachika jumla ya pointi 38 kwa AS Douanes, huku Maluach akipachika nyavuni pointi 7 na rebaundi 9 katika mechi yake ya kwanza ya BAL.

XS
SM
MD
LG