Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 21:48

Timu 8 zilizofanikiwa kuingia robo fainali ya klabu bingwa barani Afrika - BAL sasa zajulikana


Samkello Celle wa Capetown Tigers akikokota mpira kumpita mchezaji wa Al Ahly ya Misri katika mchezo wa kanda ya Nile.
Samkello Celle wa Capetown Tigers akikokota mpira kumpita mchezaji wa Al Ahly ya Misri katika mchezo wa kanda ya Nile.

Timu nane zilizofanikiwa kuingia robo fainali ya klabu bingwa barani Afrika - BAL  ya mwaka 2023 sasa zinajulikana kufuatia kumalizika kwa kanda ya Nile iliyofanyika Cairo, Misri.

Timu ya Cape Town Tigers ya Afrika Kusini walipata nafasi ya kuingia katika michuano hiyo ya mtoano itakayofanyika Rwanda Mei 20-27 baada ya kuwalaza City Oilers ya Uganda kwa jumla ya pointi 80-70 siku ya Jumamosi.

Mabingwa hao wa Afrika Kusini walitinga hatua ya mtoano kwa mara ya pili mfululizo.

Timu nyingine za kanda ya Nile zinazoelekea duru ijayo ni pamoja na mabingwa wa kanda hiyo Petro de Luanda ya Angola, Al Ahly ya Misri , na Ferroviario da Beira ya Msumbiji .

Cape Town Tigers waliingia katika mchezo wao wa mwishoni mwa juma wakiwa na kikosi kilichkosa wachezaji wao nyota.

Zaire Wade, Evans Ganapamo na Joshua Hall, wote walikaa nje katika mchezo huo mgumu kutokana na matatizo ya kiafya, lakini kikosi chao cha kilichobaki kiliibuka kidedea.

Samkelo Cele, Pieter Prinsloo na Michael Gnibjie walichukua majukumu ya kuongoza katika kuwazuia City Oilers kusonga mbele hadi kwenye michuano ya fainali.

Mfungaji bora wa Oilers James Justice Jr. Alipunguzwa kasi na kujikiuta akipata pointi 9 pekee ndani ya dakika 40 uwanjani huku Falando Jones, mchezaji pekee wa Oilers kufunga kwa tarakimu mbili, alimaliza akiwa na pointi 27.

Wakishangiliwa na mchezaji nyota wa zamani wa NBA Dwyane Wade na mkewe Gabrielle Union na idadi ya wawekezaji wa timu hiyo, Tigers ilivuka kile kilichoonekana kuwa hakiezekani na kujipatia tiketi ya kwenda michuano ya fainali Rwanda.

Cele alicheza kwa ujasiri kwa timu ya Cape Town, na kumaliza na pointi 28 katika mchezo huo.

“Ni mfungaji hodari sana; na leo tulimhitaji aongeze kasi na alielewa hilo, na ulinzi wa jumla wa timu ulikuwa wa hali ya juu” Prinsloo alisema.

Kama City Oilers wangeshinda basi wangeingia hadi raundi inayofuata, lakini, Tigers walikuwa kwenye wamejiandaa vilivyo.

"Tunaendelea kuonyesha kwamba tuna uwezo," Prinsloo alibainisha.

Aliendelea kusema: "Tulifanikiwa kumaliza na tunajisikia vizuri."

Katika mchezo wa pili wa Jumamosi Al Ahly waliifunga SLAC kwa jumla ya pointi 80-70.

XS
SM
MD
LG