Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:16

Mapigano yautikisa mji wa Khartoum baada ya afueni ya saa 24


Moshi waonekana ukitandaa mjini Khartoum, wakati wa mapigano ya Juni 4, 2023.
Moshi waonekana ukitandaa mjini Khartoum, wakati wa mapigano ya Juni 4, 2023.

Milio ya risasi na mizinga imesikika tena Jumapili katika mji mkuu wa Sudan wa Khartoum, baada ya muda wa saa 24 wa sitisho la mapigano kumalizika, mashahidi wamesema.

Mapigano mabaya yamelikumba taifa hilo la Kaskazini mashariki mwa Afrika tangu katikati ya mwezi Aprili wakati mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani Mohamed Hamdan Dagalo anayeongoza kikosi cha dharura (RSF) waliposhambuliana.

Hayo ndio makubaliano ya hivi karibuni ya kusitisha mapigano kati ya mengine kadhaa yaliyokiukwa yaliwaruhusu raia waliokwama katika mapigano hayo katika mji mkuu Khartoum, kutoka nje na kununua chakula na bidhaa nyingine msingi.

Lakini dakika 10 tu baada ya muda wa sitisho la mapigano kumalizika saa kumi na mbili asubuhi Jumapili majira ya huko, mji mkuu ulitikiswa tena na mizinga na mapigano, mashahidi wameliambia shirika la habari la AFP.

Milio ya mizinga mizito ilisikika mjini Khartoum na mji wake pacha wa Omdurman kaskazini mwa nchi, na mapigano yalizuka pia kwenye barabara ya Al-Hawa, ambayo ni barabara kuu ya kusini mwa Khartoum, mashahidi wamesema.

Forum

XS
SM
MD
LG