Watu kadhaa wamejeruhiwa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Jumatano wakati polisi wa kutuliza ghasia walipotawanya kwa nguvu maandamano ya upinzani yaliyopigwa marufuku, ambao wanatoa wito wa kufanyika tena kwa uchaguzi mkuu wa wiki iliyopita.
Upigaji kura wenye mzozo unatishia kuiyumbisha zaidi Kongo ambayo ni maskini, na tayari inakabiliwa na mgogoro wa usalama mashariki ambao umekwamisha maendeleo katika nchi hiyo yenye uzalishaji mkubwa wa madini ya cobalt na madini mengine ya viwandani na shaba.
Polisi walizingira makao makuu ya Martin Fayulu, mmoja wa wapinzani watano wa Rais Felix Tshisekedi ambao walikuwa wametoa wito kwa wafuasi wao kuandamana mjini Kinshasa siku ya Jumatano, dhidi ya uchaguzi wa rais na wabunge, ambao wanasema ulikuwa wa udanganyifu na unapaswa kufutwa. Utawala wa Tshisekedi umepuuzilia mbali madai hayo.
Tshisekedi “hakushinda uchaguzi, ushindi wake ni wa udanganyifu,” alisema mwandamanaji mmoja, ambaye alitaja jina lake kama Jean-Pierre.
Forum