Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 11:08

Ivory Coast yafuzu kuingia fainali, kukutana na Nigeria Jumapili


Mchezaji wa timu ya DRC Gedeon Kalulu (Kushoto) amenyana na mchezaji wa Ivory Coast #27 Lazare Amani wakati wa mechi ya nusu fainali za kombe la Afrika (AFCON) 2024 katika uwanja wa Alassane Ouattara, nchini Ivory Coast.
Mchezaji wa timu ya DRC Gedeon Kalulu (Kushoto) amenyana na mchezaji wa Ivory Coast #27 Lazare Amani wakati wa mechi ya nusu fainali za kombe la Afrika (AFCON) 2024 katika uwanja wa Alassane Ouattara, nchini Ivory Coast.

Kocha wa Ivory Coast Emerse Fae, alielezea ushindi wa timu yake kwenda hadi fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kuwa "kama ndoto" baada ya wenyeji hao wa michuano ya mwaka 2024 kuwalaza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 1-0 katika mechi ya mchujo Jumatano.

Sebastien Haller alifunga bao pekee la ushindi dakika ya 65 katika uwanja wa Ebimpe Olympic, na kuivusha Ivory Coast hadi fainali Jumapili dhidi ya Nigeria.

Ilikuwa hatua ya kustaajabisha kwa Ivory Coast, ambao walikuwa kwenye ukingo wa kuondolewa baada ya kufungwa 4-0 na Equatorial Guinea, kwenye uwanja huo huo, kwenye mechi yao ya Januari 22.

Fainali ya Jumapili itakuwa na taswira ya marudio ya mchuano wa makundi kati ya Ivory Coast na Nigeria, wa Januari 18, ambapo Super Eagles walishinda 1-0.

Wakati huo huo, DR Congo italazimika kuwania nafasi ya tatu mjini Abidjan Jumamosi dhidi ya Afrika Kusini.

Walikuwa na matumaini ya kushinda hadi fainali ya kwanza ya Kombe la Mataifa tangu wawe mabingwa, wakati huo nchi yao ikijulikana kama Zaire, mwaka 1974, nusu karne iliyopita.

Jumatano, Nigeria walifuzu kkuingia fainali baada ya timu yao Super Eagles kuwacharaza Bafana Bafana ya Afrika Kusini, mabao manne kwa mawili, kupitia mikwaju ya penalti.

Forum

XS
SM
MD
LG