Uganda inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa rais na bunge hapo Januari 14 2021. Kuna wagombea 11 wanaopigania kiti cha rais ambapo Rais wa sasa Yoweri Museveni anagombea mhula wake wa sita.
Alipigwa risasi mara kadhaa miguuni wakati wa vita lakini akanusurika kifo, japo inaripotiwa kwamba makamanda wenzake walikuwa wamepoteza matumaini iwapo angepona.
Ametawala Uganda kwa mda wa miaka 34 (January 26, 1986 – 2020) na ana amini kwamba ndiye mtu pekee mwenye uwezo na ujuzi wa kuongoza Uganda.
Bobi Wine alichaguliwa kuwa mbunge wa Kyadondo mashariki, July 11 2017, na kuanzisha chama chake cha National unity platform NUP, ambapo wafuasi wake wanamtambua kama kiongozi wa watu wanaotaka mabadiliko nchini Uganda,
Hajawahi kufanya kazi ya kuajiriwa kulingana na maelezo yake kwani amemaliza masomo ya chuo kikuu hivi karibuni lakini alifanikiwa kuzuru kote Uganda na kupata saini za wafuasi wake na kulipa shilingi milioni 20 zinazohitajika ili kuidhinishwa kama mgombea.
Patrick Amuriat, aliteuliwa kuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Forum for democratic change, baada ya Dr. Kiiza Besigye kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho...
Ni kiongozi wa chama cha Alliance for National Transformation ANT ambacho alianzisha mwezi March mwaka 2019. Kabla ya kuunda ANT, alikuwa kiongozi wa chama cha Forum for democratic change – FDC kati yam waka 2012 na 2017.
“Hata huna ruhusa ya kunitisha wala kuninyooshea kidole. Kwa nini ufanye hivyo? Ukifanya hivyo unatafuta shida kubwa kutoka kwangu."
Muungano wa makanisa nchini Uganda unataka katiba ya Uganda kufanyiwa marekebisho na kusitisha uchaguzi wa Januari 14 ili kumruhusu rais Yoweri Museveni kuendelea kuwa madarakani kwa mda wa miaka 3 zaidi.
Kulingana na Tume ya Uchaguzi ya Uganda jumla ya watu 17,658,527 wameandikishwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021. Asilimia 76 kati ya hao ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 35, ikiwa na maana kwamba kura za vijana zinatosha kuamua uongozi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Tume ya uchaguzi imepiga marufuku kampeni za ana kwa ana katika sehemu kadhaa ambazo wachambuzi wa siasa wanasema zina ufuasi mkubwa wa mgombea wa urais Bobi Wwine.
Waandishi wamelalamika kwamba maafisa wa polisi wanawalenga wakiwa kazini, hasa wale wanaoandika habari za siasa
Karibu watu 30 waliuawa jijini Kampala na wengine zaidi ya 25 kuuawa katika miji iliyo karibu na Kampala, ya Mukono, Masaka, Luweero, Jinja, Kyotera na Rakai
Wamekubaliana pia kushinikiza jumuiya ya kimataifa kuingilia kati na kuchunguza kile wanataja kama ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu nchini Uganda unaofanywa na serikali Pamoja na wanajeshi.
Ochola ameambia waandishi wa habari kwamba “polisi wataendelea kuwapiga kwa sababu wanataka kuhakikisha kwamba hawaendi mahali kuna hatari.”
Kampuni ya facebook imefunga akaunti kadhaa zenye uhusiano na chama kinachotawala nchini Uganda cha National resistance Movement NRM.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi amesema kwamba jumla ya kura 10,359,479 zilipigwa, huku 381,386 zikiharibika.
Kwa karibu asilimia 30 ya kura zilizo hesabiwa Alhamisi, Museveni alipata kura millioni 1,852,000 sawa na asilimia 63.9, naye Bob Wine alipata kura laki 821,000 sawa na asilimia 28.4, tume ya uchaguzi nchini Uganda imesema.