Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 22:48

Dhuluma dhidi ya waandishi wa habari zaongezeka Uganda kuelekea uchaguzi mkuu


Wafuatiliaji wa uchaguzi mkuu nchini Uganda wanaripoti kuongezeka kwa hofu nchini humo kufuatia kuongezeka kwa machafuko na ukandamizaji wakati nchi hiyo inajitarayarisha kwa uchaguzi mkuu wiki ijayo, Januari tarehe 14.

Upinzani mkubwa ni kati ya rais wa sasa Yoweri Museveni na mwanamuziki ambaye pia ni mbunge Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, ambaye ana ufuasi mkubwa wa vijana.

Mkuu wa shirika la kutetea haki za waandishi wa habari nchini Uganda Robert Ssempala, amesema kwamba zaidi ya waandishi wa habari 100 wameshambuliwa tangu kampeni zilipoanza nchini humo.

Ssempala amesema kwamba matukio ya waandishi wa habari kushambuliwa vimeongezeka kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea wakati wa uchaguzi mkuu.

Amesema waandishi wa habari nchini Uganda wanapitia wakati mgumi kwa sasa wakiwa kazini.

"Tangu wagombea wa viti mbali mbali walipoidhinishwa na tume ya uchaguzi, zaidi ya wandishi wa habari 100 wamesashambuliwa. Wengine wamepigwa, wengine kupigwa risasi, vifaa vyao vya kazi kuharibiwa, magari wanamosafiria wakiwa wanafuatilia kampeni kuharibiwa.”

Serikali ya Uganda pia imeweka masharti magumu kwa waandishi wa habari ikiwemo kusajiliwa upya ndipo waruhusiwe kuandika habari za kisiasa.

"Tumeona masharti mapya yakitolewa na baraza la habari siku chache kabla ya uchaguzi kufanyika, wakitaka waandishi wote kusajiliwa upya ndipo waruhusiwe kuandika habari kuhusu kampeni. Lengo kubwa la masharti kama haya ni kuhakikisha kwamba idadi ndogo sana ya waandishi wanafuatilia uchaguzi. Tumeona waandishi wa habari kutoka nje ya nchi wakifukuzwa na kurejeshwa nchini mwao, jambo ambalo hatujawahi kuliona. Hata baadhi walizuiwa wakiwa katika uwanja wa ndege kuingia nchini.” Amesema Ssempala.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG