Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 05:48

Mkuu wa polisi Uganda asema polisi wataendelea kuwapiga waandishi wa habari


Polisi wakikabiliana na waandishi wa habari - Uganda
Polisi wakikabiliana na waandishi wa habari - Uganda

Wakuu wa usalama nchini Uganda wameonya wapiga kura nchini humo kutosalia katika kituo cha kupiga kura baada ya kupiga kura yao.

Uganda inafanya uchaguzi mkuu alhamisi wiki ijayo.

Kampeni za uchaguzi zimeshudia machafuko, vifo na kukamatwa kwa wafuasi na wagombea wa upinzani.

Wagombea wa upinzani wamekuwa wakiambia wafuasi wao kutoondoka kwenye vituo vya kupigia kura baada ya kupiga kura ili kuzuia wizi wa kura.

Mkuu wa Polisi Martin Okoth Ochola, amesema kwamba “polisi wamekuwa wakishambulia waandishi wa habari wakati wa kampeni ili kuwazuia kufikia sehemu kulipo na hatari.”

Ochola ameambia waandishi wa habari kwamba “polisi wataendelea kuwapiga kwa sababu wanataka kuhakikisha kwamba hawaendi mahali kuna hatari.”

Baadhi ya wandishi wanaendelea kuuguza majeraha baada ya kushambuliwa na wanajeshi.

Tume ya uchaguzi imetangaza kwamba wapiga kura wote wanastahili kuondoka vituo vya kupiga kura baada ya kupiga kura.

Kamera na simu havitaruhusiwa katika vituo vya kupigia kura.

Wakati huo huo, wakili wa mgombea wa urais Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, amesema kwamba maafisa wa kampeni wa mgombea huyo wanazuiliwa katika kambi za jeshi hata baada ya mahakamama kuagiza kwamba waachiliwe huru.

Bobi Wine amesema kwamba atawasilisha malalamishi katika mahakama ya ualifu ya kimataifa ICC, kuhusu dhuluma zinazoendelea nchini humo.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA,Washington DC

XS
SM
MD
LG