Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 19:18

Uganda: Mgombea urais anyunyuziwa pilipili machoni, waandishi wa habari wagoma


Mgombea wa urais kupitia chama cha Forum for democratic change FDC Patrick Amuriat, amenyunyuziwa pilipili machoni kiasi cha kulazwa hospitalini.

Msafara wa Amuriat ulizuiwa na polisi alipokuwa safarini kwenda katika mkutano wa kampeni wilyani Tororo.

Amuriat, alifungua dirisha la gari lake kuzungumza na polisi, kwenye barabara ya Bugiri kuelekea Tororo, na ndipo afisa wa polisi kwa jina Abraham Asiimwe alipochukua fursa hiyo kumnyunyuzia pilipili machoni.

Tume ya uchaguzi imepiga marufuku kampeni katika wilaya ya Tororo, ambayo wachambuzi wa siasa Uganda wanasema ni ngome ya mgombea huyo wa upinzani. Tume hiyo inasema wilaya ya Tororo ina maambukizi mengi ya virusi vya Corona na kampeni haziweki kufanyika wilayani humo.

Nyumbani kwa Amuriat ni wilayani Tororo.

Waandishi wa habari wagoma

Waandishi wa habari wamesusia kikao na maafisa wa ngazi ya juu wa usalama wakilalamikia ukandamizaji wa polisi na wanajeshi dhidi yao.

Waandishi wamelalamika kwamba maafisa wa polisi wanawalenga wakiwa kazini, hasa wale wanaoandika habari za siasa.

Wandishi walitaka msemaji wa jeshi Brig Flavia Byekwaso kuwaomba msahama kabla ya kuwahutubia kuhusu maandalizi ya kusherehekea siku ya wanajeshi Uganda maarufu Tarehe sita.

Byekwaso hata hivyo amekatakaa kuomba msamaha na hivyo kupelekea waandishi kuondoka katika kikao hicho.

Maafisa wengine wa usalama akiwemo Maj Gen. Henry Matsiko nao wamekataa kuomba msamaha.

“Hatutaandika habari kuhusu maafisa wa usalama hadi mtakapotuheshimu na kuheshimu kazi yetu.” Mmoja wa waandishi wa habari amesema.

Hatua ya waandishi hao inafuatia tukio la jumapili ambapo polisi walishambulia na kuwajeruhi waandishi wa habari kadhaa waliokuwa wanafuatilia kampeni ya mgombea wa urais Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, katika wilaya ya Masaka.

Kikao cha mahakama kusikiliza ombi la kuachiliwa kwa dhamana wakili Opiyo chaahirishwa.

Mahakama jijini Kampala imeahirisha kusikilizwa kwa ombi la kutaka wakili wa kutetea haki za kibinadamu Nicholas Opiyo kuachiliwa kwa dhamana hadi jumatano, Desemba tarehe 30.

Opiyo anazuiliwa gerezani baada ya kufunguliwa mashtaka ya utakatishaji wa fedha.

Kikao cha leo kimesfanyika kwa njia ya video kutoka gereza la Kitalya.

Upande wa mashtaka unataka mda zaidi kuendelea na uchunguzi huku wakili wa Opiyo David Mpanga akisema kwamba Opiyo ameendelea kuzuiliwa bila kufunguliwa mashtaka na kwamba madai dhidi yake na hali ya kuendelea kuzuiliwa, inaonekana kama hatua ya kumuadhibu tu kwa kutetea haki za kibinadamu nchini Uganda.

Museveni akutana na balozi wa Marekani

Rais Yoweri Museveni amefanya kikao na balozi wa Marekani nchini Uganda Natalie E Brown, nyumbani kwa Museveni Rwakitura, magharibi mwa Uganda.

Japo Museveni ameandika ujumbe wa twitter akisema kwamba mkutano huo umekuwa wa kibinafsi, balozi Brown ameandika ujumbe wa twitter kwamba mkutano kati yake na Museveni “umeangazia uhusiano kati ya Uganda na Marekani, mazingira yanayohitajika kwa Uganda kuku ana kuvutia waekezaji, ambayo ni Pamoja na kufanyika uchaguzi wa amani, huru na haki Pamoja na mashirika ya kijamii yaliyo huru kufanya kazi zake.”

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG