Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 21:42

Akaunti kadhaa za Facebook, Twiter za chama kinachotawala Uganda zafungwa


Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na mgombea wa urais Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine (kulia)
Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) na mgombea wa urais Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine (kulia)

Facebook imesema kwamba akaunti hizo zina lengo la kueneza habari za uongo wakati nchi hiyo inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu alhamisi wiki hii.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, mkuu wa mawasiliano wa kampuni ya facebook katika kanda ya Sahara Kezia Anim, amesema kwamba akaunti hizo za facebook zilikuwa zinaeneza habari zisizo za kweli ili kubadili mawazo ya wapiga kura.

Amesema kwamba akaunti zilizofungwa zilikuwa feki, na zilikuwa zinaeneza habari za uongo hasa za kushambulia wagombea wa upinzani.

Watumiaji pia walikuwa wakitumia maudhui yanayowekwa kwenye mtandao na wagombea wa upinzani kwenye ukurasa huo na kubadilisha yaonekane kama yao Pamoja na kuongeza ndani habari za uongo na kuchafua wenzao sifa.

Kulingana na kampuni ya facebook, watumiaji wa akanuti hizo walikuwa wanazitumia kushambulia watu wengine kwa matusi na maneno makali kwenye kurasa zao na walikuwa wanatumia internet ya wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia ya Uganda.

Vyombo vya habari Uganda zinaripoti kwamba zaidi ya akaunti 100 za facebook zimefungwa.

Mkuu wa mawasiliano wa rais Yoweri Museveni, Don Wanyama, ameshutumu kampuni za facebook na Twitter akidai kwamba zinashirikiana na wanasiasa wa upinzani dhidi ya chama cha NRM.

Wanyama ameandika ujumbe wa twitter akisema kwamba akaunti zote za facebook na twitter ambazo zimefungwa zinastahili kufunguliwa, akitaka tume ya mawasiliano nchini Uganda UCC, kuhakikisha kwamba kuna usawa wa kutumia mitandao ya kidigitali nchini humo.

Wanyama amenukuliwa na gazeti la Daily Monitor akisema kwamba ni aibu kubwa wa kwatu kutoka nje ya nchi kujaribu kuweka utawala wao nchini Uganda kwa kufunga akaunti za facebook na twitter za chama cha NRM. Amesisitiza kwamba rais Yoweri Museveni hataondolewa madarakani.

Mmoja wa wasimamizi wa habari wa chama cha NRM Ashburg Kato, ameshutumu mgombea wa urais Bobi Wine kwa kushiriki katika kufunga akaunti za chama kinachotawala cha NRM.

Msemaji wa chama cha National unity platform NUP, chake Bobi Wine, Joel Senyonyi amekanusha madai kwamba wamehusika katika hatua ya kufungwa kwa akaunti hizo.

Hatua ya facebook, inajiri siku chache baada ya serikali ya rais Yoweri Museveni, kupitia tume ya mawasiliano UCC, ikitaka kampuni ya google kufunga channeli zote za You tube za wagombea wa upinzani hasa Bobi Wine. Google ilikataa kutekeleza ombi hilo.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG