Warussia walikuwa wanashukiwa wanaweza kuwachukua watoto yatima na kuwapeleka Russia, kwa hiyo wafanyakazi wa hospitali ya watoto mjini Kherson walianza kutengeneza rekodi za afya za kughushi za yatima hao ili ionekane kama vile walikuwa na hali mbaya hawawezi kuhamishwa.
“Tulifanya hilo kwa makusudi kuandika habari za uongo kuwa watoto hao walikuwa wagonjwa na hawawezi kusafirishwa,” alisema Dkt Olga Pilyarska, mkuu wa kitengo cha wagonjwa mahututi. “ Tulikuwa tunaongopa kuwa (Warrusia) wanaweza kugundua … (lakini) tuliamua kwamba tutaweza kuwaokoa watoto hao kwa gharama yoyote.”
Katika kipindi chote cha vita Warussia wamekuwa wakituhumiwa kuwasafirisha watoto wa Ukraine huko Russia au katika maeneo yanayoshikiliwa na Russia ili wawalee kama watoto wao. Takriban watoto 1,000 walichukuliwa kwa nguvu kutoka mashuleni na vituo vya yatima katika mkoa wa Kherson katika kipindi cha miezi minane ya ukaliaji mabavu wa eneo hilo, mamlaka za kieneo zimesema. Haijulikani mahali walipo watoto hao.
Lakini wakazi wanasema hata hivyo watoto zaidi wangeweza kutowekakama isingekuwa juhudi za baadhi yao katika jamii hiyo ambao walihatarisha maisha yao kuwaficha watoto wengi kadiri walivyoweza.
Katika hospitali huko Kherson, wafanyakazi walizua maradhi kwa watoto 11 waliokuwa wanwahudumia, ili wasiweze kuwatoa kwenda katika nyumba za yatima ambapo walitambua kuwa wangeingizwa katika rekodi ya Warrusia na kuwepo uwezekano mkubwa wakuchukuliwa.
Mtoto mmoja alikuwa “ anavuja damu katika moyo”, mwingine “alikuwa na degedege isiyodhibitika” na mwingine alikuwa anahitaji “kifaa cha kupumulia,” alisema Pilyarska kuhusu hizo eikodi walizotengeneza za uongo.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.
Facebook Forum