Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 17:00

EU kuunda mahakama maalum ya kuchunguza uhalifu unaodaiwa kufanywa na Russia nchini Ukraine


Rais wa Kamisheni ya EU Ursula von der Leyen akizungumza kwa njia ya mtandao, kwenye uzinduzi wa mkutano wa kimataifa kuhusu "Wazo la Ulaya'', mjini Kaunas, Lithuania, Novemba 25, 2022. Picha ya AP
Rais wa Kamisheni ya EU Ursula von der Leyen akizungumza kwa njia ya mtandao, kwenye uzinduzi wa mkutano wa kimataifa kuhusu "Wazo la Ulaya'', mjini Kaunas, Lithuania, Novemba 25, 2022. Picha ya AP

Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema leo Jumatano, kwamba Umoja wa Ulaya utajaribu kuunda mahakama maalum inayoungwa mkono na Marekani, kuchunguza na kuhukumu vitendo vya uhalifu wa vita ambavyo vinadaiwa kutendwa na Russia nchini Ukraine.

von der Leyen amesema, “wako tayari kuanza kufanya kazi pamoja na Jumuia ya kimataifa ili kupata uungwaji mkono mkubwa wa kimataifa kwa ajili ya mahakama hii maalum,”.

Ukraine imekuwa ikihimiza kuundwa kwa mahakama hii maalum kuwashtaki viongozi wa kijeshi na kisiasa wa Russia inayowatuhumu kuanzisha vita.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita yenye makao yake mjini the Hague (ICC) ilianzisha uchunguzi wake kuhusu madai ya uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita siku kadhaa baada ya uvamizi wa Moscow wa Februari 24, lakini haina mamlaka ya kushtaki uvamizi nchini Ukraine.

Russia ambayo imeziita harakati zake nchini Ukraine kuwa “operesheni maalum ya kijeshi”, ilikanusha kuwalenga raia.

XS
SM
MD
LG