Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 15:19

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza: Sababu zilizopelekea Russia kupunguza mashambulizi dhidi ya Ukraine


Maryna Semeniuk akitembea katika eneo mbele ya nyumba yake katika kijiji cha Vysoke, mkoa wa Kherson, Ukraine, Dec. 3, 2022.
Maryna Semeniuk akitembea katika eneo mbele ya nyumba yake katika kijiji cha Vysoke, mkoa wa Kherson, Ukraine, Dec. 3, 2022.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema Jumatatu kuwa idadi ya mashambulizi ya anga ya kimkakati  yanayofanywa na majeshi ya Russia dhidi ya Ukraine “yamepungua kwa kiwango kikubwa” pengine “ni kwa makumi kwa siku, ikilinganishwa yalivyokuwa juu hadi 300 kwa siku.

Katika habari zake za kijasusi za hivi karibuni, zilizobadikwa katika Twitter, wizara hiyo imesema Russia ilikuwa imepoteza zaidi ya ndege 60 za kivita.

Kupungua kwa mashambulizi, wizara hiyo ilisema, “inawezekana ni matokeo ya vitisho vya juu vinavyoendelea kutoka kwa ulinzi wa anga wa Ukraine, kikwazo cha saa ambazo ndege za Russia zinaweza kuruka, na hali mbaya ya hewa.”

“Kutokana na mashambulizi ya kimkakati ya ardhini yanayofanywa na Russia yanategemea kuyaona maeneo na pia kutumia silaha zisizo na shabaha, jeshi la anga la Russia huenda linaendelea na kiwango cha chini cha mashambulizi kutokana na hali ya hewa mbaya wakati huu wa baridi,” wizara ya hiyo ya Uingereza ilieleza.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema katika hotuba ya kila siku Jumapili kwamba Ukraine ina kitu ambacho Russia hawana.

“Tunaitetea nchi yetu na hilo linatupa motisha wa hali ya juu. Tunapigana kwa ajili ya uhuru na hilo linaongeza mara kadhaa nguvu yoyote ile. Tunatetea ukweli na hili linaiunganisha dunia kuwa pamoja na Ukraine.

Kiongozi huyo wa Ukraine pia amewasihi wananchi wa ukraine kusaidiana “kuweza kuvuka kipindi hiki cha baridi.” Alisema, “naomba usijiulize kama aunaweza kusaidia na kwa namna gani. Saidia pale unapoona unaweza kufanya hivyo.”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema Jumapili kuwa gharama inayoingia Russia kutokana na vikwazo vya Magharibi inaongezeka kila siku, ikiwawia vigumu Moscow kupata silaha zaidi ili kuendeleza vita vinavyoendelea na Ukraine.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, Reuters na AFP.

XS
SM
MD
LG