Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 18:29

Biden na Macron waapa kuiwajibisha Russia kwa vitendo vyake nchini Ukraine


Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Ufaransa Emmanuel kwenye mkutano na waandishi wa habari White House, Disemba 1, 2022. Picha ya Reuters
Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Ufaransa Emmanuel kwenye mkutano na waandishi wa habari White House, Disemba 1, 2022. Picha ya Reuters

Marais wa Marekani na Ufaransa wamesema wataiwajibisha Russia kwa vitendo vyake nchini Ukraine, huku Umoja wa Ulaya ukifikia makubaliano ya muda juu ya kikomo cha bei ya mafuta ili kubana mapato ya mauzo ya nje ya Moscow.

Joe Biden alipokutana na Emmanuel Macron huko White House alisema ana nia ya kuzungumza moja kwa moja na Rais Vladimir Putin kuhusu kumaliza vita vya Ukraine lakini hakuna dalili kwamba hilo litafanyika.

Mwezi Machi, mwezi mmoja baada ya uvamizi wa Russia, Biden alimuita Putin “mchinjaji” kutokana na vitendo vyake na kusema kiongozi huyo wa Kremlin “hawezi kubakia madarakani”.

Leo, baada ya zaidi ya miezi tisa ya vita na majira ya baridi kushika kasi, mataifa ya magharibi yanajaribu kuongeza msaada kwa Ukraine, huku ikikabiliwa na mashambukizi ya makombora na ndege zisizo na rubani (drones) ambazo zimewaacha mamilioni ya watu bila vifaa vya kuleta joto ndani ya nyumba, bila umeme na maji.

Russia iliishtumu Marekani na NATO kwa kuwa na jukumu la moja kwa moja na hatari katika vita hivyo na kusema Washington imeigeuza Kyiv kuwa tishio la muda wote kwa Moscow ambalo haiwezi kulipuuza.

Katika jitihada za kupunguza pesa zinazopatikana kutokana na juhudi za kivita za Moscow, Umoja wa Ulaya ulikubaliana kwa muda jana Alhamisi juu ya bei ya kikomo ya dola 60 kwa pipa moja la mafuta ya Russia yanayopitishwa baharini, kulingana na vyanzo vya wanadiplomasia.

Lakini hatua hiyo inahitaji kuidhinishwa na serikali zote za Umoja wa Ulaya kwa utaratibu wa maandishi kufikia leo Ijumaa.

XS
SM
MD
LG