Biden hata hivyo amesema kwamba hajaona ishara za Putin kuwa tayari kumaliza vita hivyo ambavyo vimeingia mwezi wa 10.
Katika kikao na waandishi wa habari katika White house, akiwa na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Biden amesema kwamba yupo tayari kuzungumza na Putin, lakini kwa ushauri ya nchi wanachama wa NATO.
Biden amekuwa akizungumza baada ya kufanya mazungumzo na mwenzake wa Ufaransa kwa saa kadhaa.
Ameongezea kwamba hana mipango ya haraka ya kuzungumza na Putin na hatafanya hivyo kivyake na kwamba kuna njia moja pekee ya kumaliza vita vya Ukraine, ambayo ni Russia kuacha vita na kuondoka nchini humo.
Macron amesema kwamba ana Imani kwamba Marekani itaendelea kusaidia Ukraine na silaha pamoja na msaada wa kibinadamu.