Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 08:40

Blinken asema kwamba vikwazo vya kimataifa vinaendelea kuumiza Russia


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema Jumapili kwamba vikwazo vya mataifa ya Magharibi kwa Russia vinaongezeka kila siku, na kupelekea kuwa vigumu kwa taifa hilo kutengeneza silaha zaidi ili kuendeleza vita vya Ukraine.

Wakati Russia ikiwa imewekewa vikwazo vya kibiashara na Marekani pamoja na washirika wake, Blinken amesema kwamba haiwezi kuagiza bidhaa muhimu za kukarabati au kutengeneza silaha zilizoharibiwa wakati wa vita, huku baadhi ya silaha na vifaru vikiachwa na wanajeshi wake baada ya kukabiliwa vikali na vikosi vya Ukraine.

Blinken aliyekuwa akizungumza na televisheni ya CNN katika kipindi cha State of the Union pia amesema gharama inaendelea kuongezeka kwa Russia, huku mzigo ukiendelea kuwa mzito kwa taifa hilo. Amesema kwamba washirika wa magharibi wanaendelea kutathmini vikwazo zaidi ili kudumaza juhudi za Russia hata zaidi.

XS
SM
MD
LG