Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 04:24

Stoltenberg: Russia haiwezi kuzuia nchi yoyote kujiunga na NATO


Rais wa Russia Vladimir Putin cakiongoza kikao kuhusu maendeleao mjini Moscow, Nov 21, 2022
Rais wa Russia Vladimir Putin cakiongoza kikao kuhusu maendeleao mjini Moscow, Nov 21, 2022

Mkuu wa muungano wa nchi za NATO Jens Stoltenberg amesema kwamba Ukraine ambayo sasa inapigana na wanajeshi wa Russia walioivamia, itajiunga na NATO katika siku zijazo licha ya pingamizi za rais wa Russia Viladimir Putin.

Stoltenberg ameambia mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi wanachama kwamba NATO ipo tayari kukaribisha uanachama wa Ukraine.

Mkutano huo umefanyika Romania, kujadili namna ya kuendelea kutoa msaada wa silaha kwa Ukraine. Ukraine ilituma maombi ya kutaka kujiunga na NATO mara kwanza mwaka 2018.

Amesema kwamba North Macedonia na Montenegro wamejiunga na muungano huo ulioanzishwa baada ya vita vya pili vya dunia, na kwamba Sweden na Finland zitajiunga hivi karibuni, akisisitiza kwamba Russia haina uwezo wowote wa kuzuia nchi hizo kujiunga na NATO.

Stoltenberg amesema kwamba rais Viladimir Putin hana uwezo wowote wa kuzuia nchi zenye uhuru wake kufanya maamuzi yake na ambayo sio tishio kwa usalama wa Russia na kwamba Putin anaogopa ukuaji wa demokrasia na uhuru wa nchi.

XS
SM
MD
LG