Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 07:59

Ukraine yatoa wito kiwanda cha makombora cha Russia kuwekewa vikwazo


Russian ikijaribu makombora ya nyuklia.
Russian ikijaribu makombora ya nyuklia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alisema Alhamisi alikuwa ametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kukiwekea vikwazo kiwanda cha utengenezaji makombora cha Russia.

Kuleba alitweet akisema uzalishaji wamakombora ya Russia “lazima usitishwe.” Alisema amefikisha ujumbe huo katika mkutano wake na mkuu wa sera za mambo ya nje wa Ulaya Josep Borrell na pia ameishukuru EU kwa kuipatia Ukraine msaada wa ulinzi.

Russia imekuwa ikitumia makombora kuishambulia miji ya Ukraine, ikiwemo mashambulizi katika maeneo ya miundombinu kama vile sehemu za njia kuu za umeme nchini humo.

Jeshi la Ukraine limesema Alhamisi kuwa majeshi ya Russia yalikuwa yanashambulia kwa mabomu miji kadhaa katika mkoa wa Donetsk mashariki ya Ukraine, ikiwemo mijiya Bakhmut, Soledar na Opytne.

Mkuu wa Majeshi ya Vikosi vya Ulinzi vyaUkraine pia alisema Russia ilikuwa inatumia vifaru na makombora kulenga maeneo ya Ukraine katika mji wa kusini wa Kherson.

Marekani ilisema Jumatano kuwa kampeni ya wiki nzima ya mashambulizi inayofanywa na Russia katika miundombinu muhimu ya Ukraine ya mifumo ya joto, umeme na maji haitapunguza uamuzi wanchi za Magharibi kuendelea kuisaidia Kyiv katika vita vyake vya kujihami dhidi uvamiziwa Moscow.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, kufuatia mkutano wa NATO wa siku mbili huko Bucharest, Romania, alisema katika mkutano wa vyombo vya habari kuwa Rais wa Russia Vladimir Putin alikuwa amejikita ‘vita na hasira” zake dhidi ya raia wa Ukraine wakati kipindi kikali cha baridi kikiwa kimeshawasili.

“Mfumo wa Joto, maji na umeme – hayandiyo malengo ya Rais Putin. Anashambulia vikali sana. Ukatili huu unaofanywa dhidi ya watu wa Ukraine ni wakinyama,” Blinken alisema.

Baadhi ya taarifa katika repoti hii chanzo chake ni mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

XS
SM
MD
LG