Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 02:29

Wanajeshi wa Russia 'wanajitayarisha kukiachilia' kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia


kiwanda cha Nyuklia cha Zaporizhzhia karibu na Enerhodar, eneo la Zaporizhzhia. Kiwanda hicho kinashikiliwa na wanajeshi wa Russia Okt. 14, 2022.

Mkuu wa shirika la nyuklia nchini Ukraine Petro Kotin, amesema kwamba kuna ishara kwamba wanajeshi wa Russia wanajitayarisha kuondoka kutoka kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia ambacho wamekuwa wakikishikilia tangu mwezi Machi baada ya kuivamia nchini hiyo.

Endapo hilo litatokea, itakuwa mabadiliko makubwa katika vita vya Ukraine katika sehemu za kusini mashariki mwa eneo la Zaporizhzhia ambako wanajeshi hao hawajabadilisha sehemu wanazozishikilia kwa muda wa miezi kadhaa.

Makombora ya kila mara karibu na kiwanda hicho cha Nyuklia, yalipelekea kuwepo wasiwasi mkubwa kuhusu uwezekano wa janga kubwa la Nyuklia endapo kiwanda kingeharibiwa.

Russia na Ukraine wamekuwa wakishutumiana kwa miezi kadhaa kwa kurusha makombora karibu na kiwanda cha Zaporizhiizhia, ambacho kwa sasa hakizalishi nishati.

Wanajeshi wa Ukraine wamefanikiwa kuudhibithi mji wa Kherson mwezi huu, pamoja na sehemu kubwa ya ukingo wa kulia wa Dnipro, mashariki mwa Zaporizhzhia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG