Tangazo hilo limetolewa pembeni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa wanachama wa NATO huko nchini Romania. Maafisa wa ngazi ya juu wa Marekani wamesema kwamba msaada huo utakuwa wa kutosha bila kutoa maelezo zaidi juu ya kiwango na hali ya msaada wenyewe.
Marekani pia inatarajiwa kuwarai washirika wengine wa Ukraine, kuepuka tatizo la umeme ambao ni muhimu zaidi wakati huu msimu wa baridi kali unapoanza. Wakati huo huo katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg Jumanne kwenye kikao hicho cha mawaziri cha siku mbili amesema kwamba muungano huo utaendelea kusimama na Ukraine,