Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 00:51

Pendekezo la Russia kufunguliwa mashtaka limeasilishwa UN


Wanajeshi wa Ukraine wakiendesha vifaru vilivyowachwa na wanajeshi wa Russia Oct 28,2022
Wanajeshi wa Ukraine wakiendesha vifaru vilivyowachwa na wanajeshi wa Russia Oct 28,2022

Umoja wa mataifa umeasilisha pendekezo jipya la kutaka mahakama maalum ya kimataifa kufungua kesi ya dhidi ya Russia kwa kuvamia Ukraine.

Pendekezo hilo limepokelewa kwa hisia tofauti, Ukraine na watetezi wa haki za kibinadamu wakiunga mkono huku wataalam wakieleza kukosa Imani iwapo litafanikiwa.

Mkuu wa tume ya umoja wa ulaya Ursula Von der Leyen amesema kwamba ni lazima Russia ilipie uhalifu wa kutishina ikiwemo uhalifu wa kuvamia nchi huru.

Tayari mahakama ya uhalifu wa kimataifa ICC, yenye makao yake Uholanzi, unachunguza madai ya uhalifu wa kivita, na uhalifu dhidi ya ubinadamu, unaodaiwa kutekelezwa na Russia nchini Ukraine.

Russia imekana madai ya kutekeleza uhalaifu wa kivitaa na kushutumu jumuiya ya kimataifa kwa kukosa kuzingatia kile imetaja kama dhuluma zinazotekelezwa na wanajeshi wa Ukraine.

XS
SM
MD
LG