Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 00:47

Umoja wa Ulaya wataka Russia ishtakiwe kwa uhalifu wa kivita walioufanya Ukraine


Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen akizungumza kupitia mtandao wa video katika ufunguzi wa kongamano la kimataifa juu ya fikra fikra ya Ulaya "The idea of Europe" huko Kaunas, Lithuania, Ijumaa, Nov. 25, 2022.
Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen akizungumza kupitia mtandao wa video katika ufunguzi wa kongamano la kimataifa juu ya fikra fikra ya Ulaya "The idea of Europe" huko Kaunas, Lithuania, Ijumaa, Nov. 25, 2022.

Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen ameomba  Jumatano kuundwa mahakama maalum ya kuwashtaki Warussia kwa uhalifu dhidi ya Ukraine.

Von der Leyen amependekeza mahakama inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa “kuchunguza na kuishtaki Russia kwa uhalifu wa uvamizi wa kivita.”

Pia alisema Russia na madikteta wa Russia wanatakiwa kulipa gharama za kuijenga tena Ukraine kutokana na uharibifu uliofanywa na majeshi ya Russia tangu walipoivamia Ukraine mwezi Februari.

“Uhalifu wa kutisha uliofanywa na Russia hauwezi kuachwa bila ya kuadhibiwa,” von der Leyen alisema.

Alizungumza wakati mawaziri wa mambo ya nje wa NATO wanakutana huko Romania katika siku ya mwisho ya mkutano wao uliojumuisha majadiliano ya mgogoro huo na kuiunga mkono Ukraine.

Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema Jumanne Ukraine siku moja itajiunga na muungano wa kijeshi wa nchi za Magharibi ikiwa ni ukaidi wa moja kwa moja kwa Rais wa Russia Vladimir Putin.

“Milango ya NATO iko wazi, “Stoltenberg alisema, akielezea tena nia ya dhati kwa uanachama wa Ukraine uliowasilishwa mara ya kwanza mwaka 2008 lakini ulikwama tangu wakati huo. Alieleza kuwa Macedonia Kaskazini na Montenegro hivi karibuni zilijiunga na muungano wa kijeshi wa kituo kikuu cha nchi za Magharibi – baada ya Vita vya Pili vya Dunia, na kwamba Sweden na Finland watafanya hivyo siku zijazo.

“Russia haina kura ya turufu” kwa nchi kujiunga, Stoltenberg alisema. “Tunasimamia hilo, pia, juu ya uanachama wa Ukraine.”

“Rais Putin hawezi kuinyima nchi huru kufanya maamuzi yao huru ambayo siyo tishio kwa Russia,” waziri mkuu wa zamani wa Norway alisema. Nafikiri kile anachohofia ni demokrasia na uhuru, na hiyo ndiyo changamoto kubwa kwake.

Lakini Ukraine haitajiunga na NATO karibuni, ambayo kwa mujibu wa misingi ya mkataba wa jumuiya hiyo, kuna uwezekano kupeleka majeshi ya nchi wanachama 30 kuingia katika mapigano na majeshi ya Russia.

Itakuwa ni uamuzi ambao uko nje gharama za mabilioni ya dola za msaada wa kijeshi na kibinadamu uliotolewa na Marekani na washirika wake kwa serikali ya Kyiv kuwasaidia wapiganaji wa Ukraine kuitetea nchi yao.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ametangaza kuwa Marekani itaipa Kyiv msaada mwingine wadola milioni 53 kuisaidia kununua mitambo ya dharura ya umeme kufuatia mashambulizi ya anga yanayofanywa na Russia kwa wiki kadhaa yakilenga miundombinu ya Ukraine ili kuharibu mifumo ya umeme na maji wakati wa kipindi cha baridi kikianza nchini humo.

Mwanadiplomasia huyo wa juu wa Marekani alisema vifaa vitapelekwa Ukraine kwa misingi ya dharura na kujumuisha transfoma za umeme, saketi breka, vidhibiti umeme, magari na vifaa vingine muhimu.

XS
SM
MD
LG