Tahadhari za anga zilisikika kote Ukraine na maafisa waliwataka raia kwenda mahali salama ili kujikinga na kile walichosema kuwa ni mawimbi ya hivi karibuni ya mashambulizi ya makombora ya Russia tangu uvamizi wa Februari 24.
Msemaji wa jeshi la anga Yuriy Ihnat amesema “ Makombora tayari yamerushwa”.
Hapakuwa taarifa za mara moja kuhusu uharibifu au vifo, lakini maafisa walinukuliwa na vyombo vya habari vya Ukraine wakisema kuwa milipuko ilikuwa ikisikika katika baadhi ya maeneo, huku mifumo ya ulinzi ya Ukraine ikianza kufanya kazi.
Vikosi vya Russia vimekuwa vikilenga zaidi miundombinu ya nishati ya Ukraine katika wiki za karibuni huku vikionekana kushindwa kwenye uwanja wa vita, na kusababisha uharibifu wa mitambo ya umeme wakati msimu wa baridi unaanza.
Facebook Forum