Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameonya kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano na Hamas yatamalizika na mapigano makali kuanza tena huko Gaza ikiwa mateka zaidi wanaoshikiliwa na Hamas hawataachiliwa ifikapo Jumamosi.
Utawala wa Trump umewasilisha mpango wa kupunguza wafanyakazi ulimwenguni kote, kwenye miradi inayopokea misaada kutoka Marekani, kama sehemu ya kulivunja shirika la Maendeleo ya Kimataifa ya Marekani, USAID, na kusalia na takriban wafanyakazi 300.
Ikulu ya Marekani imesema Alhamisi kwamba inafanya tathmini ya kina ya malalamishi yaliyowasilishwa na China kwa Shirika la Kimataifa la Biashara, WTO.
Afisa wa ngazi ya juu wa Shirika la Afya Duniani WHO, huko Gaza amesema Alhamisi kuwa njia zaidi za kutoka zinahitajika ili kufanya uokozi wa kimatibabu kwa maelfu ya Wapalestina wakiwemo watoto ambao wanahitaji missada ya kuokoa maisha.
Marekani ina jukumu la kimkataba la kulinda mfereji wa Panama endapo utashambuliwa, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio amesema Alhamisi.
Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz, amesema leo alhamisi kwamba ameagiza jeshi kutayarisha mpango wa kuondoa idadi kubwa ya wapalestina kutoka ukanda wa Gaza kwa kutumia usafiri wa Barabara, anga au Bahari.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio Jumatano ametangaza kwamba Marekani inapanga kuunga mkono Guatemala na miradi mipya ya miundombinu pamoja na kuondolewa ushuru kwenye misaada ya kigeni ili kuimarisha ushirika wa Marekani na taifa hilo la Amerika ya Kati.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayoshughulikia wakimbizi na uhamiaji kwa pamoja Jumatano yameelezea wasi wasi wao kuhusu mpango wa Pakistan wa kuanza mchakato mpya wa kurejesha halaiki ya wahamiaji wa Afghanistan pamoja na waomba hifadhi.
Karibu watu 70 wameuwawa na wengine 50 kujeruhiwa kufuatia mapigano ya saa 24 kati ya wapiganaji wa Islamic State na vikosi vya eneo la Somalia la Puntland.
Washirika wa Marekani pamoja na mahasimu wake wote Jumatano wameshutumu pendekezo la rais wa Marekani Donald Trump kwamba Marekani ichukue udhibiti wa Gaza
Rais Donald Trump wa Marekani amesema anataka Marekani ichukue umiliki wa Gaza ikiwa ni msimamo baada ya taarifa zake za awali za kuwalazimisha wakazi wa Gaza kuhamishiwa nchi jirani za Jordan na Misri.
Takriban watu 10 Jumanne wameuwawa kwenye ufyatulianaji wa risasi kwenye kituo kimoja cha elimu kati kati mwa Sweden akiwemo mshambuliaji, maafisa wa polisi wamesema.
Rais wa Marekani Donald Trump ameendelea kusisitiza mpango wake wa kuondolewa kwa Wapalestina kutoka Gaza wakati akiwa mwenyeji wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu huko White House Jumanne.
Rais wa Marekani Donald Trump Jumatatu amesitisha kwa muda ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa kutoka Mexico na Canada zinazoingia hapa Marekani kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuzungumza na rais wa Mexico Claudia Sheinbaum na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau.
Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Kristi Noem Jumatatu ameondoa ulinzi dhidi ya kurejeshwa nyumbani kwa mamia ya watu wa Venezuela waliopo Marekani, ikiwa sehemu ya mpango wa Trump dhidi ya uhamiaji haramu.
Nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani, WHO, zitajadili kupunguza kwa sehemu ya bajeti yake, kwa dola milioni 400 kwa kuzingatia hatua ya Rais Trump kuiondoa Marekani, mfadhili wake mkuu, kutoka kwa shirika hilo,
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio Jumapili ameambia viongozi wa Panama kwamba China ina ushawishi hatari kwenye mrefeji wa Panama, na kwamba iwapo hilo halitabadishwa, basi huenda Marekani ikalazimika kuchukua hatua muhimu za kulinda haki yake ya kutumia mfereji huo.
Polisi wa Georgia Jumapili wamekamata watu kadhaa kwenye maandamano ya maelfu ya watu waliojitokeza kuitisha uchaguzi mpya wa bunge, huku wakifunga kwa muda barabara muhimu kwenye mji mkuu wa Tbilisi.
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer Jumapili amesema kuwa atazingatia kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Marekani, baada ya rais wa Marekani Donald Trump kuashiria kuwa angeweka ushuru wa juu kwa Ulaya.
Pandisha zaidi