Hayo ni kwa mujibu wa waraka uliotolewa Jumatatu.
Akifungua mkutano wa mwaka wa bodi ya watendaji wa shirika hilo, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, pia alitetea kazi ya shirika hilo na mageuzi ya hivi karibuni na akasisitiza wito kwa Marekani kutathmini upya hatua kuondoka kwake na kuingia kwenye mazungumzo na WHO kuhusu mabadiliko zaidi.
"Tungekaribisha mapendekezo kutoka kwa Marekani, na mataifa yote wanachama, kwa jinsi tunavyoweza kukuhudumia wewe na watu wa dunia, vyema zaidi," alisema.
Kupunguzwa kwa bajeti kutajadiliwa katika mkutano wa Februari 3-11 mjini Geneva, Uswizi, ambapo wawakilishi wa nchi wanachama watajadili ufadhili wa shirika hilo na kazi yake, kwa kipindi cha 2026-2027.
Bodi kuu inapendekeza kupunguza sehemu ya bajeti za programu msingi, kutoka dola bilioni 5.3 hadi bilioni 4.9, kulingana na waraka uliotolewa Jumatatu.
Hiyo ni sehemu ya bajeti pana ya dola bilioni 7.5 ya 2026-2027 ambayo ilipendekezwa hapo awali, ikijumuisha pesa za kutokomeza polio na kushughulikia dharura.
Forum