Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 25, 2025 Local time: 04:55

Mashirika ya UN yalalamikia hatua ya Pakistan ya kurejesha maelfu ya wahamiaji wa Afghanistan


Picha ya maktaba ya wakimbizi wa Afghanistan wakisafirishwa kutoka Pakistan Novemba 3, 2023.
Picha ya maktaba ya wakimbizi wa Afghanistan wakisafirishwa kutoka Pakistan Novemba 3, 2023.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayoshughulikia wakimbizi na uhamiaji kwa pamoja Jumatano yameelezea wasi wasi wao kuhusu mpango wa Pakistan wa kuanza mchakato mpya wa kurejesha halaiki ya wahamiaji wa Afghanistan pamoja na waomba hifadhi.

Taarifa hiyo imekuja wiki moja baada ya Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif kuidhinisha mpango unaolenga karibu raia milioni 3 wa Afghanistan wanaoishi nchini humo. Kundi hilo linajumuisha wakimbizi waliyopo huko kihalali, wale wasiyo na stakabadhi pamoja na wale wanaosubiri ahadi ya kupelekwa Marekani pamoja na kwenye mataifa mengine ya magharibi.

Mpango huo ambao ulionyeshwa VOA unatoa idhidni ya kuondolewa mara moja kwa rais wa Afghanistan kutoka kwenye mji mkuu wa Islamabad pamoja na mji wa karibu wa Rawalpindi hadi kwenye makambi maalum, kabla ya kurejeshwa Afghanistan.

Waraka huo ambao haujatoa muda wa kutekelezwa kwa zoezi hilo pia unasema kuwa hakuna tangazo la umma litakalotolewa kuhusiana na upelekaji huo. Kwenye taarifa ya pamoja ya Jumatano, UNHCR, na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, walisema kuwa wanatafuta ufafanuzi kuhusu mikakati itakayotumika ukiwemo muda kwenye zoezi hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG