Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 24, 2025 Local time: 00:26

Marekani yasema ina jukumu la kulinda mfereji wa Panama


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio (Kushoto) akiwa na Rais wa Jamhuri ya Dominica Luis Abinader, mjini Santo Domingo, Alhamisi. Februari 6, 2025. (Picha ya Mark Schiefelbein / POOL / AFP)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio (Kushoto) akiwa na Rais wa Jamhuri ya Dominica Luis Abinader, mjini Santo Domingo, Alhamisi. Februari 6, 2025. (Picha ya Mark Schiefelbein / POOL / AFP)

Marekani ina jukumu la kimkataba la kulinda mfereji wa Panama endapo utashambuliwa, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio amesema Alhamisi.

Hilo limejiri wakati kukiwa na hali ya sintofahamu pamoja na kile Panama imesema ni 'uongo' kuhusu iwapo meli za kivitia za jeshi la wanamaji la Marekani zinaweza kutumia mfereji huo bila kulipia ada. “ Naona ikiwa hali tatanishi kwamba tunalipia ada kutumia mfereji huo ambao tuna jukumu la kulinda. Hayo ndiyo matarajio yetu, na yanaeleweka vyema kwenye mazungumzo hayo”, Rubio alisema wakati akizungimza na wanahabari kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Dominica wa Santo Domingo.

Rubio alifanya mazungumzo na rais wa Panama Jose Raul Mulino hapo Jumapili. Waziri huyo aliambia wanahabari kwamba ingawa anaheshimu serikali ya Panama iliyochaguliwa kidemokrasia na kutambua kuwa ina sheria inazohitajika kufuata, mkataba wa kulinda mrefeji huo ni lazima utekelezwe na jeshi la Marekani na hasa kikosi cha wanamaji. Ameongeza kusema kuwa Marekani inazingatia suluhisho la kidiplomasia na Panama kuhusu suala hilo. Rais Munilo kupitia ujumbe wa X alisema kuwa anapanga kufanya mazungumzo na mwenzake wa Marekani Donald Trump baadaye leo Ijumaa.

Forum

XS
SM
MD
LG