Mwanahabari mmoja wa shirika la habari la Reuters alishuhudia waandamanaji watatu wakikamatwa akiwemo Nika Melia, ambaye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Coalition for Change. Shirika la habari la Interfax limesema kuwa Melia baadaye aliachiliwa kwa dhamana baada ya kuzuiliwa kwa muda. Hakukuwa na ripoti yoyote kutoka kwa polisi, lakini wizara ya usalama wa ndani ilisema kupitia taarifa kabla ya maandamano hayo kwamba polisi wangehakikisha kwamba maandamano hayo yanafanyika kwenye mazingira ya amani na kwa mujibu wa sheria.
Meya wa zamani wa Tbilisi Giorgi Ugulava pia alikamatwa wakati wa maandamano hayo, vyombo vya ndani ya habari vimesema. Mkuu wa sera za kigeni kwenye Umoja wa Ulaya Kaja Kallas, Jumapili alikemea ukamataji huo. “Msako mkali dhidi ya waandamanaji , wanahabari na wanasiasa nyakati za usiku mjini Tbilisi haukubaliki, Kallas aliandika kwenye ukurasa wake wa X. Aliongeza kusema kuwa Georgia haijakidhi viwango kama taifa linalotaka kujiunga na EU. Wakazi wa Georgia wamekuwa wakiandamana nyakati za usiku tangu Novemba baada ya chama tawala cha Georgian Dream kusema kuwa kinasitisha mazungumzo kuelekekea kujiunga na EU, hadi 2028.
Forum