Shirika hilo limewaajiri maelfu ya wafanyakazi. Jana Alhamisi, vyama vya wafanyikazi wa serikali kuu viliwasilisha kesi mahakamani, kuitaka kusitisha mpango wa kufungwa kwa shirika hilo, vikisema kwamba Rais Donald Trump hana mamlaka ya kuvunja idara ambayo iliundwa na sheria ya bunge.
Wafanyakazi wawili wa sasa wa USAID na afisa mmoja mkuu wa zamani wa shirika hilo walilielezea shirika la habari la The Associated Press kuhusu mpango huo wa serikali ya Trump, uliowasilishwa kwa maafisa wakuu waliosalia kwenye shirika hilo.
Walizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao kutokana na agizo la utawala wa Trump linalowazuia wafanyakazi wa USAID kuzungumza na mtu yeyote nje ya shirika lao.
Mpango huo utawaacha chini ya wafanyakazi 300 kazini, kati ya walioajiriwa na wanakandarasi 8,000 wa sasa.
Wao, pamoja na idadi isiyojulikana ya wafanyakazi wa kimataifa walioajiriwa ndani na nje ya nchi, wanatarajiwa kuendesha programu chache tu za kuokoa maisha ambazo utawala wa Trump unasema unanuia kuendelea nazo kwa sasa.
Forum