Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 20:41

Shirika la mpango wa Chakula Duniani WFP limeanza kusambaza chakula cha msaada Tigray


Wafanyakazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wakipita mbele ya magunia ya ngano yaliyokuwa kwenye ghala huko Adama, Ethiopia, Januari 12, 2023. Picha na Amanuel Sileshi / AFP.

Shirika hilo la msaada wa Chakula la Umoja wa Mataifa lilisema limeanza kusambaza magunia ya ngano ya kilo 15 yaliyopakiwa awali kwa zaidi ya watu 100,000 kama sehemu ya mradi wa majaribio.

Shirika la mpango wa Chakula Duniani –WFP lilisema Jumanne kwamba limeanza kusambaza chakula cha msaada katika eneo lililokumbwa na vita la Tigray nchini Ethiopia katika jaribio la hatua mpya za ufuatiliaji.

WFP na Shirika la misaada ya Chakula la Marekani -USAID walisitisha msaada wa chakula kwa nchi hiyo ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika mwezi Juni baada ya kugundua kuwa vyakula hivyo haviwafikii walengwa na hivyo kuzua hofu kwamba mamilioni ya Waethiopia wangeachwa katika hali mbaya.

Siku ya Jumanne shirika hilo la msaada wa Chakula la Umoja wa Mataifa lilisema limeanza kusambaza magunia ya ngano ya kilo 15 yaliyopakiwa awali kwa zaidi ya watu 100,000 kama sehemu ya mradi wa majaribio na mifumo iliyoboreshwa ya ufuatiliaji.

Forum

XS
SM
MD
LG