Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 06, 2025 Local time: 15:23

Maelfu ya raia wa Venezuela kwenye hatari ya kurejeshwa makwao kutoka Marekani


Wahamiaji kutoka mataifa mbalimbali wanaojaribu kuingia Marekani wakiwa Mexico City Juni 6, 2024. PIcha na Yuri CORTEZ / AFP.
Wahamiaji kutoka mataifa mbalimbali wanaojaribu kuingia Marekani wakiwa Mexico City Juni 6, 2024. PIcha na Yuri CORTEZ / AFP.

Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Kristi Noem Jumatatu ameondoa ulinzi dhidi ya kurejeshwa nyumbani kwa mamia ya watu wa Venezuela waliopo  Marekani, ikiwa sehemu ya  mpango wa Trump dhidi ya uhamiaji haramu.

Uamuzi huo una maana kwamba takriban watu 348,000 kutoka Venezuela waliyopo kwenye program maalum inayotoa vibali vya muda vya kuishi Marekani huenda wakarejeshwa makwao au kupoteza vibali vya kufanya kazi ifikapo Aprili, kulingana na ilani iliyotolewa na serikali.

Ilani hiyo imesema kuwa vibali hivyo ni kinyume na maslahi ya Marekani, na kwamba haviendani na hali iliyopo Venezuela. Vibali hivyo kwa kawaida hutolea kwa watu ambao nchi yao imekumbwa na janga asilia, ghasia au tukio jingine lisilo la kawaida. Rais wa Marekani Donald Trump baada ya kuapishwa Januari 20 aliahidi kukabiliana na uhamiaji haramu pamoja na program za kibinadamu ambazo anasema haziendani na sheria za Marekani.

Wakati wa muhula wake wa kwanza, alijaribu kusitisha program ya utoaji wa vibali vya muda, lakini mahakama za serikali zilizimamisha zoezi hilo. Rais aliyeondoka madarakani Joe Biden alikuwa amepanua program hiyo inayotoa vibali vya muda kwa zaidi ya watu milioni moja kutoka mataifa 17. Baadhi yao wameishi Marekani kwa miongo kadhaa lakini sasa wapo kwenye hatari ya kurejeshwa makwao.

Forum

XS
SM
MD
LG