Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 16, 2025 Local time: 18:43

China yawasilisha malalamishi dhidi ya Marekani kwa WTO


Mkuu wa WTO Ngozi Okonjo-Iweala akizungumza na wanahabari kwenye makao makuu mjini, Geneva Februari 16, 2024.
Mkuu wa WTO Ngozi Okonjo-Iweala akizungumza na wanahabari kwenye makao makuu mjini, Geneva Februari 16, 2024.

Ikulu ya Marekani imesema Alhamisi kwamba inafanya tathmini ya kina ya malalamishi yaliyowasilishwa na China kwa Shirika la Kimataifa la Biashara, WTO.

Malalamishi hayo yanashutumu Marekani kwa kutoa madai ya “uongo na yasiyo na msingi,' kuhusu jukumu la China kwenye biashara ya dawa ya kulevya ya fentanyl, kama kigezo cha kuweka ushuru kwenye bidhaa za China.

Malalamishi hayo yaliwasilishwa Jumatano siku moja baada ya rais wa Marekani Donald Trump kuongeza ushuru wa asilimia 10 kwenye bidhaa kutoka China. Ikulu ya Marekani imesema kuwa ushuru huo mpya unalenga kusitisha uingizaji wa fentanyl pamoja na kemikali husika Marekani.

China kwa upande wake imesema kuwa itaweka ushuru mpya wa asilimia 10 kwa bidhaa za Marekani, pamoja na asilimia 15 kwa makaa ya moto, gesi asilia na asilimia 10 kwenye vifaa vya kilimo na magari yanayotoa moshi mwingi.

Taifa hilo pia lilipiga marufuku upelekaji wa baadhi ya madini muhimu, wakati pia likianzisha uchunguzi dhidi ya kampuni kubwa ya teknoojia ya Marekani ya Google. Kwenye malalamishi yaliowasilshwa kwa WTO, China imesema kuwa ushuru wa Marekani ni wa kibaguzi na unalenga kujilinda huku ukihujumu sheria za kimataifa za biashara.

Forum

XS
SM
MD
LG