“Kunahitaji kuwa na jinsi ya kuwawezesha wagonjwa zaidi kupitia Rafah kuingia Misri, lakini pia tunahitaji njia nyingine,” Dkt Rik Peeperkorn aliambia wanahabari kwa njia ya video kutoka Gaza. “Njia ya kwanza ambayo tungependa kuona ikifunguliwa tena ni ile ya kitamaduni kwelekea Ukingo wa Magharibi na mashariki mwa Jerusalem.
Hospitali za mashariki mwa Jerusalema na Ukingo wa Magharibi zipo tayari kupokea wagonjwa. Peeperkorn alisema kwamba chini ya makubaliano ya sitisho la mapigano, hadi wagonjwa 50 wa Kipalestina wakiwa wa wenzao wanaweza kuokolewa kutoka Gaza kila siku.
Kufikia sasa hawajaweza kuokoa zaidi ya wagonjwa 39 kwa siku. Amesema kuwa ni lazima hali iimarishwe kwa wagonjwa 12,000 hadi 14,000 wanaohitaji kuokolewa wakiwemo watoto 5,000. Baadhi ya wagonjwa wapo kwenye hali ya mshituko, matatizo ya moyo na wengine saratani.
Forum