Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 06:07

Guatemala yakubali kupokea maelfu ya wahamiaji kutoka Marekani


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio (Kushoto) na Rais wa Guatemala Bernardo Arevalo mjini Gutemala City, Jumatano Feb 5, 2025.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio (Kushoto) na Rais wa Guatemala Bernardo Arevalo mjini Gutemala City, Jumatano Feb 5, 2025.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio Jumatano ametangaza kwamba Marekani inapanga kuunga mkono Guatemala na miradi mipya ya miundombinu pamoja na kuondolewa ushuru kwenye misaada ya kigeni ili kuimarisha ushirika wa Marekani na taifa hilo la Amerika ya Kati.

Akizungumza wakati wakiwa na rais wa Guatemala, Bernardo Arevalo mbele ya wanahabari, Rubio alisema alitia saini barua inayounga mkono ahadi ya ushirikiano kamili na wizara ya mambo ya nje kwenye ushirikiano wa wahandisi wa kijeshi wa Guatemala na Marekani.

Miradi iliyopo ni kuanza mpango wa awali wa kupanuliwa kwa bandari mbili mpya pamoja na barabara kuu na reli, ili kuweka Guatemala kwenye viwango vya nchi muhimu ya kibiashara na kuongeza nafasi za kiuchumi. Guatemala imefikia makubaliano mapya ya uhamiaji na Marekani, ambayo yataruhusu ndege zaidi za raia wake wanaorejeshwa kutoka Marekani, rais Arevalo alitangaza Jumatano baada ya kikao chake na Rubio.

“Kwenye mpango huo, tumekubali kuongeza kwa asilimia 40, safari za ndege zinazorejesha wahamiaji, wale wa Guatemala na mataifa mengine, rais Arevalo alisema kupitia mkalimani. Alifafanua kuwa makubaliano hayo na Marekani yatahakikisha usalama na ubinadamu wa watu watakaorejeshwa kutoka Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG