Jeshi la Israel limesema mateka wanane, wakiwemo Waisraeli watatu na raia watano wa Thailand, waliachiliwa Alhamisi huku Israel na Hamas wakifanya ubadilishanaji wa tatu wa mateka na wafungwa chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano ya zaidi ya miezi 15 huko Gaza.
Idara kadhaa za Marekani zimeanzisha uchunguzi kujua chanzo cha kugongana kwa ndege ya abiria ya shirika la American Airlines na helikopta ya jeshi la Marekani karibu na Washington Jumatano usiku.
Ndege ya abiria iligongana na helikopta ya kijeshi ya Marekani Jumatano usiku wakati ilipokuwa inakaribia kutua kwenye uwanja wa ndege wa Washington DC Reagan National, Mamlaka ya usafiri wa anga FAA ilisema.
Kesi iliwasilishwa Jumanne kwenye mahakama ya serikali kuu jijini Washington kwa niaba ya mashirika yasiyo ya faida, wamiliki wa biashara ndogo ndogo na wataalamu wa afya ya umma, saa chache kabla ya amri ya kusitishwa kwa fedha za ufadhili wa serikali kuu kuanza kutekelezwa.
Maelfu ya Wapalestina walimiminika kuelekea Gaza city Jumatatu, huku Israel ikifungua vituo vya ukaguzi na kuwaruhusu watu kurejea katika maeneo ya kaskazini mwa eneo hilo ambalo lilikuwa limefungwa tangu siku ya mwanzo ya vita kati ya Israel na Hamas, zaidi ya miezi 15 iliyopita.
Jumuia ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC imelaani “kitendo cha uvamizi cha waasi wa M23 wanaoendesha harakati zao mashariki mwa DRC.
Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu alisema kwamba mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la Congo katika mji mkuu muhimu wa mashariki mwa nchi yalikuwa “hayajamalizika”, licha ya waasi hao kudai kwamba waliuteka mji wa Goma.
Wakuu wa Nchi na serikali 5 za Afrika wamekutana jijini Nairobi Jumatatu kujadilia marekebisho ya kitaasisi ya Umoja wa Afrika, AU, na kukubaliana kuhusu haja ya kuharakisha mageuzi ya kuwezesha AU kutekeleza vipaumbele vyake bila kutegemea fedha za kigeni.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema Alhamisi kwamba hivi karibuni atazungumza na mwezake wa Russia Vladimir Putin ili kujaribu kumshinikiza amalize vita vilivyodumu kwa karibu miaka mitatu na jirani yake Ukraine.
Wabunge wa Marekani Alhamisi wamewasilisha msuada unaolenga kusitisha hadhi maalum ya kibiashara kwa China na Marekani, kuongeza ushuru kwa kiwango cha juu, pamoja na kumaliza sera ya kutolipiwa ushuru kwa bidhaa za thamani ndogo kutoka China.
Hata kabla ya kuwepo ofisini kwa saa 48, rais wa Marekani Donald Trump alituma ujumbe wa kukabiliana na China kwenye anga za juu, na kwamba utawala wake utakuwa na ajenda kubwa ifikapo kuendesha Marekani mbele kwenye teknolojia ya akili mnemba au AI pamoja na miundombimu inayoiendesha.
Mamlaka za California Jumatano zimetoa amri ya watu kuondoka kwenye maeneo ya ndani baada ya moto mpya kuzuka ukiwa na upepo mkali kwenye milima iliyopo kasakzini mwa Los Angeles.
Pentagon itaanza kupeleka hadi wanajeshi 1,500 ili kusaidia kulinda mpaka wa kusini na Mexico katika siku za karibuni.
Maafisa wa Uturuki wamesema Jumanne kwamba moto kwenye hoteli yenye ghorofa 12 katika mji maarufu wa kitalii kaskazini magharibi wa nchi umeua takriban watu 76, wawili miongoni mwao wakiwa ni kutokana na kuruka kutoka jengo hilo baada ya moto kuzuka.
Makundi ya Wakurdi nchini Syria yameelezea matumaini yao kwamba Marekani itaendelea kuwaunga mkono wakati rais mpya Donald Trump anapoanza kuhudumu kwenye muhula wa pili.
Viongozi mbali mbali wa mataifa Jumatatu wameendelea kumpongeza rais mpya wa Marekani Donald Trump, kufuatia kuapishwa kwake kama rais wa 47.
Rais mpya wa Marekani Donald Trump Jumatatu usiku baada yakuapishwa mchana alikutana na maelfu ya wafuasi wake kwenye ukumbi wa Capitol One Arena mjini Washington DC.
Donald Trump ameapishwa leo Jumatatu kuchukua rasmi hatamu za uongozi kama rais wa 47 wa Marekani. Kurejea kwake madarakani ni tukio la kihistoria kwa mtu ambaye katika kipindi cha zaidi ya miaka tisa alikibadili chama cha Republican katika nchi inayozidi kukumbwa na migawanyiko.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump Jumapili amewahutubia maelfu ya wafuasi wake kwenye jiji kuu la Marekani Washington akiwaahidi kuchukua hatua kali dhidi ya uhamiaji.
Uingereza na Ukraine Alhamisi zilisaini makubaliano ya miaka 100, huku Uingereza ikiahidi kuipa Ukraine msaada wa kijeshi wa dola bilioni 3.6 mwaka huu.
Pandisha zaidi