Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 27, 2025 Local time: 12:54

Gaza: Wanajeshi wa Israel kutayarisha mpango wa kuwahamisha Wapalestina


Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi Israel Katz.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi Israel Katz.

Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz, amesema leo alhamisi kwamba ameagiza jeshi kutayarisha mpango wa kuondoa idadi kubwa ya wapalestina kutoka ukanda wa Gaza kwa kutumia usafiri wa Barabara, anga au Bahari.

Katz amekubaliana na kile rais wa Marekani Donald Trump alitaja kuwa mpango mahsusi kwa ajili ya wakaazi wa Gaza, kuondoka ukanda huo ambao umeharibiwa na mashambulizi ya Israel dhidi ya wanamgambo wa Hamas.

Maafisa wa Palestina wamekataa pendekezo la Trump alilotoa Jumanne wakati wa mkutano na waandishi Habari aliyofanya pamoja na Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Rais Trump alisema kwamba Marekani itachukua usimamizi wa Ukanda wa Gaza na kuwalazimisha Wapalestina milioni 2 kuhamia nchi nyingine na kubadilisha Gaza kuwa mandhari ya kitali ya Riviera huko mashariki ya kati.

Netanyahu aliliambia shirika la habari la Fox News jana Jumatano kwamba Wapalestina wanaweza kuondoka Gaza wakati inajengwa upya na kurudi baadaye.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Rais wa Marekani Donald Trump wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari ukumbi wa East Room huko White House, Jumanne, Feb 4, 2025, Washington, DC.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Rais wa Marekani Donald Trump wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari ukumbi wa East Room huko White House, Jumanne, Feb 4, 2025, Washington, DC.

Donald Trump, Rais wa Marekani alisema: "kila mtu niliyezungumza naye amelipenda wazo la Marekani kumiliki eneo hilo, kulijenga na kubuni maelfu ya nafasi za ajira, na kulibadili kuwa la kuvutia ambalo hakuna atakayelitambua.

Hakuna mtu anayetaka kuliangalia kwasababu wanachoona ni vifo na uharibifu na vifusi."
Trump alitoa tangazo hilo baada ya kumkaribisha Waziri mkuu wa Israel Benjamina Netanyahu huko White House.
Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel: "Nimesema hili hapo kabla. Ninasema tena Wewe ndiye rafiki mkubwa wa Israel kuwahi kuwepo hapa White House."
Trump hakufafanua jinsi anavyopanga kuchukua udhibiti wa Gaza eneo ambalo limeharibiwa na miezi 15 ya vita. Hakufuta uwezekano wa kupeleka wanajeshi wa Marekani. Haiko bayana kuikalia Gaza kutaingiliana vipi na lengo la Trump mwenyewe la kupanua mkataba wa Abraham kuihusisha Riyadh. Mkataba ambao aliousimamia ambao ulianzisha uhusiano kati ya Israel na nchi za Kiarabu mwaka 2020.

Forum

XS
SM
MD
LG