Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 06, 2025 Local time: 15:20

Marekani yasitisha kwa muda ushuru mpya dhidi ya Mexico na Canada


Picha yenye bendera za Marekani, Canada na Mexico.
Picha yenye bendera za Marekani, Canada na Mexico.

Rais wa Marekani Donald Trump Jumatatu amesitisha kwa muda ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa kutoka Mexico na Canada zinazoingia hapa Marekani kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuzungumza na rais wa Mexico Claudia Sheinbaum na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau.

Sheinbaum alisema kuwa atatuma kikosi cha wanajeshi 10,000 ili kukabiliana na tatizo la uingizaji wa dawa ya kulevya aina ya fentanyl Marekani. “Mexico itaweka doria kwenye mpaka wa kaskazini ili kuzuia ulanguzi wa dawa kutoka Mexico, na hasa fentanyl, “Sheinbaum alisema kupitia ujumbe wa X, baada ya kufanya mazungumzo na Trump.

“Marekani imeahidi kusitisha upelekaji haramu wa silaha hatari Mexico,” Sheinbaum aliongeza kusema. Kiongozi huyo wa Mexico alisema kuwa mataifa yote mawili yataendelea kushauriana kwenye masuala ya usalama, biashara na kwamba ushuru uliotangazwa awali umesitishwa kwa mwezi mmoja.

Trudeau kwa upande wake alisema kuwa Canada itatumia teknolojia mpya pamoja na wafanyakazi kwenye mpaka wake na Marekani ili kuhakikisha usafirishaji wa fentanyl unasitishwa. White House haikusema lolote, ingawa Trump aliambia wanahabari kwamba mazungumzo yake ya simu na Trudeau yalikwenda vizuri.

Forum

XS
SM
MD
LG