Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:53

Rais wa Ufaransa kuzuru Afrika

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katikati, akipiga picha baada ya mchezo wa mpira wa vikapu wakati wa kilele cha mkutano wa Afrika na Ufaransa mwaka 2021, uliofanyika katika jiji la Montpellier lililopo kusini mwa Ufaransa. Octoba 8, 2021. Picha na Ludovic MARIN / AFP.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atazuru Afrika wiki hii katika ziara ya kukabiliana na ushawishi wa Russia unaotishia kuvuruga mikakati ya Ufaransa barani Afrika.

Ziara ya Macron inajiri baada ya Ufaransa kukumbana na changamoto za kijeshi na kisiasa katika nchi washirika barani Afrika, katika siku za karibuni.

Macron atatembelea nchi za Congo Brazaville, Gabon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na Angola.

Ziara yake inajiri wakati kuna matamshi ya chuki dhidi ya Ufaransa katika eneo la Sahel.

Burkina Faso iliwafukuza wanajeshi wa Ufaransa wiki chache zilizopita na kumaliza ushirikiano wake wa kijeshi na Ufaransa katika kupambana na makundi ya wanajihadi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Burkina Faso inakuwa nchi ya hivi punde kukataa msaada wa Ufaransa, ambayo iliwaondoa wanajeshi wake kutoka Mali mwaka uliopita baada ya viongozi wa kijeshi kuanza ushirikiano na mamluki kutoka Russia na kumaliza muongo mzima wa operesheni zake dhidi ya waasi wa kiislamu.

XS
SM
MD
LG