Wiki hii tunaangazia mkutano kati ya rais wa Russia Vladimir Putin na viongozi wa nchi za Afrika, mapinduzi nchini Niger na Maandamano nchini Israel. Mtayarishaji na msimulizi wa kipindi ni Kennes Bwire
Viongozi wa Afrika wanaanza mkutano wao na rais wa Russia Vladmir Putin, nchini Russia lakini chini ya nusu ya marais wa Afrika wanahudhuria mkutano huo wakisema wanastahili kuakilishwa na mwenyekiti wa umoja wa Afrika hatua ambayo Russia inadai inachochewa na nchi za magharibi.
Lugha za asili barani Afrika ni vyema zitumike katika kuboresha msamiati wa Kiswahili ili kuendelea kukikuza na kutumika katika nyanja mbali mbali ikiwemo katika fani za sayansi na teknolojia.
Shirika la afya duniani WHO, na washirika wake wamesema kwamba karibu dozi milioni 18 za chanjo ya kwanza ya malaria duniani, zitatolewa kwa nchi 12 za Afrika ifikapo mwaka 2025.
Rais wa Kenya William Ruto ametia saini kuwa sheria mswada wa kwanza wa fedha wa serikali yake, unaolenga kuongeza mapato kwa kutoza kodi katika bidhaa kadhaa bila kujali ukosoaji kwamba ongezeko hilo la kodi litasababisha matatizo mengi zaidi ya kiuchumi kwa wananchi.
Jeshi la Sudan limekabiliwa na mashambulizi kutoka sehemu mbali mbali siku ya Jumatatu baada ya kupoteza udhibiti wa makao makuu ya polisi kwa wanamgambo wakati wa mapigano Jumapili katika mji mkuu wa Khartoum, yaliyosababisha vifo vya takriban watu 14
Jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia linashuhudia upungufu mkubwa wa chakula kwa karibu miaka miwili sasa. Lakini hali imekua mbaya zaidi tangu mashirika ya misaada ya dharura kusitisha kwa muda ugawaji wa chakula kutokana na tuhuma za utumiaji mbaya wa misaada ya chakula inayotolewa.
Familia za waathiriwa wa mkasa mbaya kabisa kutokea katika pwani ya Kenya, kwenye shamba la Shakahola ambako watu walidanganywa na mchungaji wao kubaki na njaa hadi kufariki ili kuweza kwenda kukutana na Yesu, wanedelea kuomboleza vifo vya wapenzi wao.
Milipuko ilitikisa miji mkuu wa Sudan wa Khartoum siku ya Alhamisi, miezi miwili zaidi baada ya mapigano kuzuka kati ya majenerali hasimu nchini, huku kila upande ukimshutumu mwingine kwa mashambulizi dhidi ya raia.
Rais Joe biden ametoa wito wa kuwepo na uhuru wa kuabudu kwa misingi ya haki kwa india na Marekani alipokua anamkaribisha Waziri mkuu wa india Narenda Modi White House Alhamisi.
Mapigano makali yamezuka kati ya makundi hasimu ya kijeshi katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Sudan siku ya Jumatano, wakati sitisho la mapigano la saa 72 lilipomalizika ambapo baadhi ya riporti zimedai kuwepo kwa ukiukwaji wa makubaliano hayo, mashuhuda walisema.
Waziri wa biashara wa Kenya yuko katikati ya mivutano mikali kutokana na mfululizo wa matamshi ya dharau dhidi ya chombo kikubwa cha habari, ikiwa ni pamoja na kuwaita waandishi wa chombo hicho kuwa ni "makahaba."
Pandisha zaidi