Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 04:19

M23 wanaendelea kudhibithi sehemu zaidi Mashariki mwa DRC


Kanali John Imani Nzenze (katikati), kamanda wa kundi la waasi la M23
Kanali John Imani Nzenze (katikati), kamanda wa kundi la waasi la M23

Mapigano makali yanaendelea Kivu kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya jeshi la serikali FARDC na waasi wa kundi la M23.

Waasi wa M23 wameuteka mji wenye shughuli za uchimbaji madini wa Rubaya, ulio magharibi mwa Sake na Goma.

Kulingana na ripoti ya shirika linalofuatilia mapigano ya DRC, Crisis 24, waasi wa M23 vile vile wanadhibithi miji ya Kingi na Karuba.

Waasi wa M23 waliuteka mji wa Mushaki mnamo Februari 24.

Mamia ya watu wamelazimika kuhama sehemu ambazo waasi hao wanazishikilia.

Sehemu ambazo wamezidhibithi zipo kwenye barabara kati ya Masisi na Goma, inayotumika kwa usafiri wa bidhaa kuingia Goma.

Waasi hao walichukua udhibiti wa Kitchanga Januari 26.

Mapigano yanaendelea Mweso na Kitchanga na kuzuia ufanisi kuingia Goma.

Waasi wa M23 walitakiwa kuondoka sehemu ambazo wanazishikilia kulingana na makubaliano wa viongozi wa jumuiya ya Afrika mashariki.

Waasi wa M23 wameongeza mashambulizi tangu mwezi Novemba 2021, wakilenga kambi za jeshi za serikali, mashariki mwa DRC.

Amri ya kuacha mapigano

Mapigano hayo yamepeleka mgogoro wa kidiplomasia kati ya Rwanda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. DRC inashutumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi wa M23. Rwanda inakanusha madai hayo licha ya ripoti kadhaa ikiwemo ya wataalam wa umoja wa mataifa kutaka Rwanda kuacha kuunga mkono waasi wa M23. Marekani vile vile imetaka Rwanda kuacha kuunga mkono waasi wa M23.

Mnamo Juni 2022, waasi wa M23 walidhibithi mji wa Bunagana na kuanza kupigana wakielekea Goma na wameteka sehemu kadhaa kwenye njia kuu ya kuelekea Goma.

Waasi wa M23 wanalenga kulazimisha serikali ya Kinshasa kukubali makubaliano ya amani ya mwaka 2013, wakitaka wapiganaji wake kujumuishwa katika jeshi la taifa, miongoni mwa mambo mengine.

Viongozi wa jumuiya ya Afrika mashariki wamekuwa wakiimrisha juhudi za kutaka vita hivyo kumalizika, tangu Novemba 2022 lakini waasi wa M23 wameendelea kutekeleza mashambulizi.

Kundi hilo limekuwa likitaka kufanyika mazungumzo ya moja kwa moja na serikali ya DRC ambayo imesema kwamba haiwezi kufanya maungumzo na ‘magaidi’.

XS
SM
MD
LG