Mahakama ya Uganda Jumanne ilitupilia mbali rufaa ya kundi la kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja lililotaka usajili wa serikali, na kuamua kwamba kundi hilo lina lengo la kuendeleza shughuli “haramu”.
Serikali ya Haiti iliomba rasmi msaada wa usalama kutoka kwa nchi zote kote duniani, zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Mzozo wa Israel na wanamgambo wa Hamas ulitawala katika hotuba za viongozi wa nchi wanachama wa mataifa yasiyofungamana na upande wowote yaani Non-Aligned Movement (NAM) katika kongamano la 19 la Vuguvugu hilo lililofanyika Kampala, Uganda.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na mgombea wa zamani wa urais Bobi Wine leo Alhamisi amesema polisi waliizingira nyumba yake na kumuweka “chini ya kizuizi cha nyumbani” kabla ya maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika.
Mwili wa mwanariadha Benjamin Kiplagat ulipatikana ndani ya gari Jumamosi usiku kwenye viunga vya Rift Valley katika mji wa Eldoret nchini Kenya
Jeshi la Uganda limesema limemuua kamanda wa kikosi cha kundi la waasi la Islamist rebel Allied Democratic Forces (ADF) wanaoshutumiwa kufanya mauaji mabaya ikiwemo mauaji katika shule ya bweni.
Baada ya kufuata viwango vya kimataifa, Uganda inatarajia kuondolewa katika orodha ya ‘Grey List’ ya nchi dhaifu katika sheria za kuzuia ulanguzi wa pesa haramu na ufadhili wa ugaidi mapema mwaka ujao
Wanamgambo kutoka kundi la wanajihadi la Allied Democratic Forces (ADF) limemchoma moto bibi na wajukuu zake wawili mpaka kufa siku ya Krismasi huko magharibi mwa Uganda, maafisa wa eneo hilo wamesema.
Wizara ya mafuta ya Uganda imesema Jumamosi kwamba imeongeza muda wa leseni kwa kampuni ya Nigeria ya Oranto Petroleum Limited, kwa muda wa miaka miwili zaidi.
Askofu John Promise Daniel, Makamu wa Rais wa Pentekoste Fellowship of Nigeria anasema baraka za jinsia moja, au ndoa, hazikubaliki. Wakati huo huo mwanaharakati wa Nigeria, Promise Ohiri anayejulikana kama Empress Cookie aliamka na kushangilia habari hii siku ya Jumanne.
Takriban watu watano wameuawa, akiwemo diwani, baada ya washukiwa waasi kutoka kundi la Allied Democratic Forces (ADF) lenye uhusiano na Islamic State kushambulia eneo la Magharibi mwa Uganda Jumatatu jioni, mbunge wa eneo hilo ameliambia Shirika la habari la Reuters.
Mahakama nchini Uganda leo Jumatatu imeanza kusikiliza kesi inayopinga sheria kali iliyopitishwa dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, inayotaoa hukumu ya kifo kwa baadhi ya matendo ya wapenzi hao, pamoja na hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela kwa kuendeleza ushoga.
Pandisha zaidi