Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 06, 2025 Local time: 15:33

Uganda yaaanza kutoa chanjo za Ebola kwa wakazi wake


Watu wakitembea kwenye mji mkuu wa Uganda, Kampala, ambako mlipuko wa Ebola umetangazwa.Picha ya Januari 30, 2025.REUTERS/ Abubaker Lubowa.
Watu wakitembea kwenye mji mkuu wa Uganda, Kampala, ambako mlipuko wa Ebola umetangazwa.Picha ya Januari 30, 2025.REUTERS/ Abubaker Lubowa.

Uganda Jumatatu imeanza kutoa chanjo za Ebola aina ya Sudan, ugonjwa ambao umeua mtu mmoja na kutangazwa kuwa mlipuko wiki iliyopita.

Mkuu wa shirika la kimataifa la afya WHO, Tedros Adhanon Ghebreyesus amesema Jumatatu kupitia ujumbe wa X kwamba zoezi hilo la majaribio limeanza kwa kasi kubwa ikiwa siku tatu pekee baada ya kutangazwa kwa mlipuko huo, wakati sheria zote za kimataifa na kitaifa zikizingatiwa.

Maafisa hawajatoa jina la kampuni iliyotengeneza chanjo hizo ambazo zaidi ya 2,000 zitatolewa kwa taifa hilo la Afrika Mashariki. WHO inasaidia Uganda kukabiliana na mlipuko huo kwa kutoa msaada wa dola milioni moja kutoka kwenye mfuko wake wa dharura. Kufikia sasa ni kifo kimoja tu za muuguzi mwanaume aliyekuwa akifanya kazi kwenye hospitali ya Mulango, jijini Kampala, kilichotangazwa nchini humo, kutokana na Ebola, wakati kesi nyingine mbili zikidhibitishwa Jumatatu. Shirika la habari la AP limesema kuwa kesi hizo zinahusishwa na wanafamilia wa muuguzi aliyekufa.

Kabla ya kufa, muuguzi huyo alitafuta matibabu kwenye hospitali kadhaa pamoja na daktari wa kienyeji kabla ya vipimo kudhibitisha kuwa aliugua ebola, mamlaka husika zimesema. Dkt Matshidiso Moeti mratibu wa WHO barani Afrika kupitia taarifa ya Jumatatu baada ya mlipuko huo kudhibitishwa alisema, “ Tunakaribisha kutangazwa kwa haraka kwa mpliuko huo na hatua za dharura zinachukuliwa huku tukishirikiana na serikali pamoja na washirika wengine kugundua kesi mpya , kuweka watu karantini , kutoa matibabu pamoja na kuzuia kuenea kwa virusi ili kulinda maisha ya watu.”

Forum

XS
SM
MD
LG